Thursday, July 19, 2012

Nukuu ya Leo kutoka UN

“Neither peace, development nor human rights can flourish in an atmosphere of corruption.”(Amani, maendeleo au haki za binadamu haviwezi kushamiri mahali penye ufisadi) - Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

M4C yavuna mamia Chato kwa Magufuli

Mmoja wa mavuno mapya ya M4C ni Dk. Benedict Lukanima, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe. Ndiye aliyenipokea na kunionyesha mazingira katika Chuo Kikuu cha Hull, Uingereza; wakati huo akiwa katika mwaka wa pili wa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Uchumi.

Wednesday, July 18, 2012

Nukuu ya Sugu Bungeni

"Natuma salamu kwa Kova kwamba ile filamu yake ya Dk Ulimboka, Mchungaji, na Mkenya, wananchi hawajaielewa; hivyo ni vema arudi Studio ili afanye remix!" Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema)


Sunday, July 08, 2012

Nukuu ya Leo

"Katika mapambano ya ukombozi ni lazima wengine wawe mbegu, sisi tupo tayari kufanywa mbegu.” Dk. Willibrod Slaa Julai 8, 2012: Dar es Salaam

Saturday, July 07, 2012

Libya wachagua rais mpya

Wananchi wa  Libya leo wamejitokeza kwa wingi kupiga kura kuchagua rais, katika uchaguzi huru baada ya miaka 60 ya udikteta. Habari zaidi soma hapa.

Serena ang'ara tena

Mchezaji maarufu za tenisi Serena Williams ameibuka kidedea kwa kutwaa taji mara ya tano
.

Narejea

Nimekuwa mbali na blogu hii kwa muda sasa. Nimerejea. Tarajia mwendelezo wa harakati.
My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'