Tuesday, November 21, 2006

Tazama Ubunifu


Rafiki yangu mmoja aitwaye Alex Kaija amenitumia picha hii. Nimemuuliza alikoipata akasema naye ametumiwa. Hamjui aliyeitengeneza. Nimevutiwa na ubunifu wake; nikaona vema niwashirikishe wasomaji wa blogu hii. Mnasemaje?

6 comments:

Reginald S. Miruko said...

Ubunifu huu mzuri, lakini tuachie mahakama ifanye kazi yake

Jeff Msangi said...

Nimeupenda ubunifu huu,najaribu kwa kasi kuendelea kujifunza utundu huu wa kutumia photoshop.
Hivi wananchi wakisema wanachokiamini wanazuia vipi mahakama kufanya kazi yake.Hivi mahakama zinafanya kazi kwa kutegemea sheria inavyosema au maneno ya watu?Nadhani hili suala la kusema wananchi wasiseme kitu ni kuwanyima haki yao ya kujielezea.Naona kama hili linapingana na ile ibara ya haki za raia za msingi zikiwemo za kujielezea.Au wenzangu mnasemaje?

Maggid Mjengwa said...

Jeff,
Nadhani Wananchi hawawezi kuendesha Mahakama zao sambamaba na Mahakama tulizojiwekea. Vinginevyo, tuanzishe Mahamakama za wananchi " Gachocha" kama zile za Rwanda. Bila shaka, wananchi wanaweza kutoa mawazo yao juu ya kesi husika, lakini hapaswi kutoa hukumu.

ndesanjo said...

Wananchi kutoa mawazo hatuwezi kuzuia. Hasa katika mazingira ambayo huwa inaonekana kuwa watu jela ni kwa ajili ya wavaa kandambili na kuwa sheria huwa haichukui mkondo wake inapokutana na wenye nafasi za utawala na mali. Naelewa kabisa kwanini wananchi wamekuja juu na na hata kutoa mawazo ambayo yameonekana kuwa ni kutoa hukumu. Lakini hukumu ya wananchi inafuata hisia na historia wakati hukumu ya mahakama inafuata sheria na sio maneno ya wananchi mtaani.

Lakini katika yote nashangaa kwanini leo hii ghafla tumeanza kusema eti, "ooh wananchi msihukumu." Kila siku nasoma magazeti yanasema, "Jambazi lauawa." Je sio mahakama yenye haki ya kutamka kuwa mtu ni jambazi? Au utasikia, "Kibaka achomwa moto." Je haisemekani kuwa mtu hana kosa hadi mahakama itamke? Lakini wakati wote huu hatusikii watu wakiwataka wananchi au vyombo vya habari viache kuhukumu. Au ni kwakuwa watu hawa wanaoitwa vibaka na majambazi hawana nyadhifa za juu?

Wananchi wanahukumu kwa maneno na hisia zao imeonekana kuwa ni jambo baya sana. Lakini wananchi wanapohukumu kwa kuua kwa kupiga mawe na kuchoma moto mbona hili halipigiwi kelele sana?

Sisemi wananchi wasihukumu ila tu nataka tutazame suala hili kwa kutazama pande zote za mambo kama haya kwenye jamii yetu.

ndesanjo said...

Ngurumo,
ningependa kujua aliyetengeneza picha hiyo. Tafadhali.

Anonymous said...

Picha hiyo ilitolewa toka hapa: http://www.lintukoto.net/demonstration/, au http://www.lintukoto.net/banner/

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'