
CCM walidai kwamba Mbowe alipata watu wengi kwenye kampeni kwa sababu watu walikwenda kushangaa helikopta. Nikiitazama picha hii naona jambo tofauti. Helikopta ipo uwanjani lakini hawaitazami. Wameiacha nyuma, wanamkodolea macho Mbowe (hayupo pichani). Tazama nyuso zao. Waliofuatilia kampeni zake wanajua hali ilikuwa hivyo kila mkutano wake wa kampeni Oktoba - Desemba 2005. Tazama mmoja wa washindani wake. Nimesikia watu wakijiuliza. Nami najiuliza. Na sasa nawauliza nyie wasomaji. Tuulizane. Hivi kura za Mbowe zilikwenda wapi?
1 comment:
Huwajui CCM, nini! Na ujinga wa umma ulichangia. sasa walichochagua kiko wapi? Bomu, bomu!
Post a Comment