Monday, December 04, 2006

Ahadi za JK zaanza kutekelezwa


Wakati wa kampeni za urais mwaka 2005, JK alisema: "Tanzania Yenye Neema Inawezekana." Aliahidi "kushamirisha demokrasia." Na zaidi ya yote, aliahidi "maisha bora kwa kila Mtanzania" kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya. Mwaka mmoja umepua tangu aingie madarakani. Haya ndiyo matokeo ya ahadi hizo?

2 comments:

Anonymous said...

Bwana Ngurumo, ni kweli kabisa mambo yamekwenda mrama kabisa.
Tatizo wananchi wengi mbumbumbu na vyombo vya habari(magazeti na redio) inaonekana sijui vimebanwa au kusahau kazi yao, hali halisi haielezwi na kuchambuliwa.
Huyu jamaa JK kaleta ubishoo kwenye kuongoza nchi, usanii umezidi, usikose uchambuzi wangu siku ya uhuru nitaeleza nionavyo ndani ya blogu.

Anonymous said...

"wahenga" wa zama mpya wanasema, "ahadi sio deni."

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'