Saturday, September 29, 2007

Warioba amekuwaje?


Sielewi Jaji Joseph Sinde Warioba amekuwaje. Kiongozi mstaafu, mwanasheria mstaafu na mtu aliyewahi kuongoza tume ya rushwa anaposema 'tuhuma hizi si mpya,' anataka kusema alitarajia kuona mpya zipi? Au alitaka hizi za zamani ziachwe tu? Simwelewi. Namshangaa pia anapoona kwamba kujadili rushwa ya wakubwa si muhimu kwa maendeleo ya nchi. Zaidi nipale anapopata shida kuelewa kwanini rais na rais mstaafu wanatuhumiwa. Nadhani angepaswa kuwashangaa wao na kujiuliza: "kwanini watuhumiwe? Kwanini wao na si wengine?" Badala yake, anawatetea kana kwamba anatoa 'hukumu kuwasafisha.' Bado simwelewi. Hivi hajui kwamba Tanzania itakuwapo bila yeye wala Jakaya Kikwete au Benjamin Mkapa?

13 comments:

suzan said...

Huyu naye keshachoka akili, apumzike na kula pensheni kwa amani. Siku zake za kuwa mtawala na mshauri wa wengine zimepita

Anonymous said...

Unajua kuwa sasa hivi ndio utaenda kuona watu makini na watu ambao wako katika fikra za Kimla hivyo anataka kusema kuwa watu hawa sio mwahalifu.. Je nani ajui kama sio wasafi.. Wamefanye kura ya maoni then wananchi ndio wamfanye uamuzi wa kusema kuwa nani wasafi nani sio.. Hivyo Mzee huyu naye ametumwa kuja kama kuziba midomo na kutisha watu wa kusema ukweli.. hata rais wa Marekani kama ana tuhumu huwa anaitwa na kuchorwa kikatuni hivyo sioni ajabu kuona rais kama Mungu mtu.. Ndio maana sasa hivi mambo yanakwenda vibaya wanashindwa kumwambia na kujifanya kama wanampenda kumbe sio.. Wapinzani hongera sana.. Wananchi na Watanzania ndio watasema nani mkweli nao sio. Lakini wengi wao wasema wanamiliki Nini?? Mbona mpaka leo hakuna kiongozi hata mmjoja aliyesema mali yake?? kwanini mbona mtangulizi wake alifanya hivyo. Hivyo Baadhi ya vyombo vya habari vimechagia sana kwa kuwageuza Viongozi wa CCM ni Miungu watu.. huu ni upuuzi mkubwa ndio maan unaona leo mtu akikosolewa kidogo anasema mimi ni nani mimi mtu mkubwa. Then Matatizo mengine yapo kwenye Katiba. Siyo Accountability kabisa kwa voingozi kwa kusema ukweli na kuwa Catayst ya maendeleo na viongozi. Sio wajitete wao Wananchi ndio wawatete wao.
Joshua Michael
Colorado Marekani

luihamu said...

KAKA NIMEKUSOMA NAAMINI KABISA KISWAHILI SOMO GUMU SANA.

Anonymous said...

alichojaribu kukifanya warioba ni kuwatengenezea kona wahalifu ili waichonge kufunga bao ila imeshindikana kama ulivyoona waziri wa habari na michecho kaimalizia vibaya hivyo akashtukiwa kuwa japo warioba amedai hajatumwa na mtu lakini ukweli ni huo kakubali kutumika kijinga au alikuwa anajaribu kujisafisha kiaina kwenye meremeta

Siriha said...

Warioba has no moral authority to speak for the Tanzania poor; for all along he has been a defender of "MAFISADI". During his tenure as the primeminster, he defended those who had overinvoiced and purchased a secod hand ferry for magogoni which was poularly known as 'UNIFLOAT'.He is also involved in gold peocessing company that has milked billions from BOT. As if that is not enough ,he represents Celtel International on the TTCL board of Directorss; remember this is the company that swidled us millions in the transaction to privatise TTCL!! On this basis he has no credibility to speak on our behalf.

Kalundi said...

Warioba should not lecture us on the achievements of the Mkapa presidency. We all appreciate what he did for his country.At issue currently engulfing our former President is the ownership of Kiwira coal mines!! We need an explanation as to how the transaction was carried out to hastly transfer public property to Mbuna ,Mama Mkapa and Mkapa Jr.[Nico].If Warioba wants to defend his benefactor he should address himself to this issue.

SIMON KITURURU said...

Samahani, natoka nje ya somo!

Njoo tumalizie kujadili kipengele, ili tuende kwenye hatua nyingine ya kuboresha wanajumuiya wa jumuiya ya Watanzania wanao tembelea au wanao blogi.

Tembelea hapa : http://blogutanzania.blogspot.com/
ilia tumalize kujazia dondoo ili tu anze na kipengele kingine.
Idumu JUMUWATA!

kamala J Lutatinisibwa said...

yaani ndugu ans. hii ni hatari, hawa jamaa wanajiona kuwa wao ndio tanzania, wanafikiri bado watz ni watu wa ndio mzee, hawajui huu ni ulimwengu wa ict taarifa zinasambaa bila mpaka. kazi yao ni kushirikiana kuuza nchi na kumiliki mali zetu eh?
no time to listen to them

Siriha said...

Kitururu, tafadhali usituharibie mijadala yetu kwenye blog hii. Sisi hapa tunajadili mambo serious sio kama kwenye blog zenu nyingine. Tafadhali usituchafue!!

Sarafina said...

Siriha,

Mweleze ukweli, wamezoea kuvuruga mijadala ya wenzao kama kina JK wanavyofanya sasa kujaribu kuwaondoa wananchi katikamijdala muhimu kwa mbinu mbalimbali.

kamala J Lutatinisibwa said...

hiyo ndo janja ya ccm, kotkote wapo kueneza propaganda na kupoteza mijadala ya kusema ukweli. kuna haja ya ma-blog administrator kufuta commets za hawa waeneza propaganda

Kambele said...

Ansbert na wachangiaji wengine wote naomba mnisaidie kwa kitu kinachonikwaza kidogo kuhusu tuhuma za ufisadi zinazomhusu Rais mstaafu Mkapa; anatuhumiwa kuwa mkewe, mwanae na mzazi mwenzie wamepora mali za umma za Kiwira Coal Mines. Katika daftari la msajiri makampuni JE yeye yumo?? Kama hayumo ni sahihi kumshutumu kwa makosa ya Mkewe, Mtotowake mwenye umri wa zaidi ya miaka kumi na nane na huyo mzazi mwenzie? Tafadhali msinielewe vibaya kuwa najaribu kumtetea Mkapa la hasha mimi naomba mnieleweshe.

Anonymous said...

hivi naye si mmoja wa washuri wa kampuni ya madini ya mwananchi? damu nzito kuliko maji

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'