Monday, April 07, 2008

Adui wa Kikwete si Karume


Kama Rais Jakaya Kikwete anataka kumaliza mpasuko wa kisiasa Zanzibar, huku Rais Amani Karume anakataa, na Kikwete anakubali kugomewa kama ilivyotokea Butiama majuzi; ni nani adui wake katika hili?

8 comments:

Anonymous said...

Adui wa Kikwete ni yeye mwenyewe. Basi!

Anonymous said...

Adui mkubwa wa Kikwete ni Kikwete mwenyewe na hatari kubwa kwa Kikwete ni historia yake. Aliingia kwa uongo na uongo huo huo utamdondosha muda si mrefu.
Nchi imemshinda. Ameshindwa hata kujielewa. Hana wa kumuelewa kabla ya kujielewa. Hata sisi hatumuelewi. Haeleweki na akieleweka vizuri hatabakia ikulu yetu akifanya anayofanya.

Alimtegemea Lowassa akadondoka. Anategemea uongo nao utamdondosha.

Kwa upande wa Karume hana tofauti na jini lililotolewa kwenye chupa. CCM ilimfinyanga sasa anaikanyaga!
Alitengenezwa kulinda maslahi yao wasijue anayo maslahi yake!
Walimdhania bwege naye sasa anawafanya mabwege!
Yetu macho.

Hata CUF nao wana matatizo. Wamehangaishwa kwa miaka kibao wasitie akilini. Tatizo lao ni kufanya mambo ya kisheria kienyeji na ya kienyeji kisheria.
Mwenye ufunguo wa mtafaruko ni wananchi wenyewe wenye kutatwa nao.
Tusiwaachie wanasiasa mafisadi kulhali watuamulie mstakabali wetu. Lao ni kutaa taa kulinda uoza wao. Lao ni kucheza na kalenda ili kila mmoja amalize ngwe yake ya hasara kwetu.
Ngurumo mdogo wangu nakuonea huruma kama ninavyojionea huruma. Maana tumewapa umma adui yao wameshindwa kumkabili. Lakini usiache kunena. Maana imeandikwa- heri ya kijana maskini mwenye busara kuliko mfalme mpumbavu.

Yetu kama wanafalasafa ni kunena na kunena na kunena. Tunene na kunena na kunena huenda ipo siku nyoyo, vichwa na masikio vitafunguka na kufanya la maana.
Hakika adui wa Kikwete ni Kikwete kama watanzania walivyo maadui wao wenyewe.
Mpayukaji Msemahovyo.
Sirini Kijiweni POPOTE.

Anonymous said...

Adui wa Kikwete ni Kikwete mwenyewe. kwlei kabisa

Anonymous said...

Ujumbe wa Mpayukaji ni mzito. Ni makala tosha na somo lenye kuhitaji kurasa milioni. Kwa mhutasari ameweza kutegua kitendawili kinachotusumbua. Heri naye angelijadili hili la uadui wa Karume na Kikwete.
Neneni na kunena jamani.
Sam

Simon Kitururu said...

Kazi kwelikweli!

Anonymous said...

wa kulaumiwa ni KIKWETE kwasababu yeye ni Mwenyekiti wa ccm,rais wa serikali ya jamhuri ya muungano!

kwa mamlaka/nafsi aliyonayo anaweza kushinikiza rais wa zanzibar ajiuzulu!kama alivyowahi kufanya Mwl.nyerere kwa abdul jumbe!

kwahiyo ni kikwete wa kulaumiwa kwa kushindwa kutekelezwa kwa makubaliano ya muhafaka baina ya vyama viwili vya ccm na cuf.

Anonymous said...

wa kulaumiwa ni KIKWETE kwasababu yeye ni Mwenyekiti wa ccm,rais wa serikali ya jamhuri ya muungano!

kwa mamlaka/nafsi aliyonayo anaweza kushinikiza rais wa zanzibar ajiuzulu!kama alivyowahi kufanya Mwl.nyerere kwa abdul jumbe!

kwahiyo ni kikwete wa kulaumiwa kwa kushindwa kutekelezwa kwa makubaliano ya muhafaka baina ya vyama viwili vya ccm na cuf.

Anonymous said...

Wa kulaumiwa si Kikwete, ni wananchi wenyewe wa visiwani waliomchaugua kwa kura nyingi Mh Karume wakambwaga Maalimu. Tazama sasa anataka kuingia serikalini kwa mlango wa nyuma-wa muafaka-badala ya kura. Uamuzi wa wananchi walio wengi ndiyo unaomponza Karume. Muafaka ni ndoana ya CUF, wananchi wamenga'mua;Maalimu alijua pia; ndiyo maana anaogopa kuupeleka muafaka kwa wananchi ukapewe ridhaa yao. Mjanja kweli kweli.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'