Friday, April 24, 2009

Mengi anamsaidia Rais Kikwete?

Mwenyekiti Mtenadaji wa IPP, Reginald Mengi, amelipuka na kuwasha moto mpya dhidi ya mafisadi. Kama ilivyokuwa kwa Dk. Willibrord Slaa aliyetangaza orodha ya mafisadi kwa sifa, vyeo na majina yao Septemba mwaka juzi, Mengi naye amethubutu kutaja majina matano tu ya wale aliowaita mapapa wa ufisadi nchini. Ni wazi, wengine tuliwajua mapema, walishatajwa walishanong'onwa, wana tuhuma nzito lakini kwa sababu zinazojulikan kwa watawala, mafisadi hao hawashitakiki. Baadhi yao wako mahakamani wanashitakiwa kwa ufisadi.

Wapo watu wanaombeza Mengi kwa tamko hili; na wapo wanaomuunga mkono. Wote hao, pamoja na Mengi, tutawajadili baadaye. Lakini kijumla ni kwamba, kwa maslahi yoyote yale, Mengi amethubutu. Je, unataka kuwajua 'Mapapa wa 'Mengi?' Hawa hapa. Hawa wamemnukuu lakini wakaogopa kutaja majina. Na yeye anasema kwa kauli yake hiyo anamsaidia Rais Kikwete kupambana na ufisadi. Ni kweli? Sehemu ya pili hii hapa.

1 comment:

Anonymous said...

Nikupongeze tena brother kwa makala nzuri, makini na iliojaa mashiko. Kama kawaida sijajuta kupoteza muda wangu baada ya kufika mwisho wa makala. Makala kama hizi zinawatofautisha waandishi na wababaishaji.

Nimependa pale ulipotofautisha kile alichosema Mengi na Mengi mwenyewe kitu ambacho wengi wameshindwa. Nasikia mmoja kati ya hao wa5 waliotajwa alipoulizwa kuhusu haya alijibu kwamba hajibu lolote kwani anamuheshimu Mengi kama baba yake-jamani what is this tena?? Tunazungumzia tuhuma kwamba umetuibia si heshima yako kwa Mengi. It's fun kwamba bado watz tunakubali majibu mepesi kama haya kwa maswali magumu yenye masilahi ya Taifa.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'