Wednesday, April 01, 2009

Obama atua London



Rais wa Marekani Barack Obama yupo London akiwa na mkewe Michelle kushiriki mkutano wa nchi 20 zenye nguvu zaidi kiuchumi. Huyu hapa akishuka kwenye ndege yake na kuelekea kwenye 'chopa' kwenda Ubalozi wa Marekani nchini Uingereza. Hizi hapa ndizo mbwembwe zinazoambatana na msafara wa 'kiranja wa marais' duniani (wapo katika picha ya pamoja chini kulia).

Matukio mengine: Obama, Gordon Brown na waandishi wa habari. Obama na 'Kwini.' Obama na vigogo wengine 19. Siasa za tabasamu za wake wa wakubwa (tazama picha hapo juu kushoto) na video kadhaa zinazoonyesha harakati za Michelle akiwa London - Cheki hapa na hapa. Brown akifungua mkutano. Baada ya mkutano Obama alikwenda Ufaransa, Ujerumani na nchi nyingine za Ulaya. Muone hapa akimudu jukwaa mbele ya umma Ufaransa.

No comments:

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'