Sunday, March 22, 2009

Buriani Jade Goody

MSANII maarufu wa runinga nchini Uingereza, Jade Goody, aliyekuwa anasumbuliwa na Kansa, ambaye aliolewa (shukrani zake hapa) na kubatizwa pamoja na watoto wake wawili, ameaga dunia usiku wa kuamkia leo Jumapili 22, 03, 2009. Mwanamuziki Darren Hayes amemsindikiza Jade kwa kibao cha I miss you . Humjui Jade Goody? Maelezo haya yanaweza kukusaidia kumfahamu. Alijiandalia mazishi yake mwenywe, na alitaka yawe ya kifahari, iwe hafla ya kusherehekea maisha yake mafupi ya miaka 27, hata kama yatapambwa na machozi ya baadhi ya baadhi ya waombolezaji. Apumzike kwa amani!

1 comment:

MAKULILO Jr, said...

NGURUMO,
Nakubaliana na Chaguo lako kuwa NUKTA77 ndio bora zaidi.

Unapotaka kuona Blog bora kabisa ya Kitanzania, naamini kwa wengi hii www.nukta77.blogspot.com ni THE BEST.Mimi naiukubali sana Blog yenyewe, pia DA SUBBI kwa moyo wake wa kuendeleza blog hiyop, na moyo wake wa ukarimu wa kugawa ujuzi bure kupitia Falsasa ya PUGU. Ukifungua blog ya NUKTA, nenda usome falsafa hii kiundani.

Mimi kwa kuona umuhimu wa blog hii, nimeipa heshima ya kipekee ktk blog yangu WWW.MAKULILO.BLOGSPOT.COM kwa kiweka kabisa pale juu ktk titles.Ni yeye aliyenibadilishia muonekano wa blog yangu wa almost 90% naweza kusema in terms of its appearance and layout, mimi ni just mbwembwe kidogo tu niliweka.

Ikitokea tunatafuta BLOGA BORA YA KITANZANIA hii NUKTA 77 kwa mtazamu wangu pia, naamini wengi walio nahatika kufika ktk blog hii watakubalina nasi Ngurumo.

Mungu akupe nguvu zaidi Da Subi.Akuzidishie moyo wa upendo ndugu.

Ngurumo, nashukuru kwa mtazamo wako khs NUKTA77 ambao nilishawahi kumwandikia e-mail kuhusu huu mtazamo wangu pia.

MAKULILO Jr,
www.makulilo.blogspot.com

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'