My Photo
Ansbert Ngurumo
Maisha yangu yamezungukwa na kuchongwa na Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo; siogopi wala kupendelea au kubagua binadamu yeyote. Tatizo langu: sivumilii ujinga na sina utii wa kikondoo kwa wenye mamlaka. Kuhoji na kudadisi ni sehemu ya maisha yangu itokanayo na hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'
View my complete profile

Saturday, June 27, 2009

Serikali inataka kulikoroga jeshi letu?



Serikali imeamua kulipaka jeshi letu matope ya ufisadi, kulifanya ngao ya ufisadi wa vigogo, huku ikisisitiza kwamba ni kwa maslahi na usalama wa taifa. Je, inajua madhara yake? Ni haki kulitumia jeshi letu kulinda matumbo machafu ya wanasiasa? Huu ndio mjadala wa Maswali Magumu wiki hii.