Friday, February 11, 2011

Kikwete anawajua Dowans

HOJA yangu ni kwamba Rais Jakaya Kikwete na serikali yake wanawajua Dowans kabla hata hawajarithi mkataba wa Richmond. Wanajua kuwa wanasheria wetu ndio walioandika mkataba huo; ndio waliotushauri kuuvunja; na ndio waliotutetea tukashindwa. Kauli ya sasa ya Rais Kikwete kwamba hawajui Dowans ni ya kujikosha, na ya kisaliti kama ya Mtume Petro, mbele ya kijakazi, dhidi ya Yesu. Blogu hii inajua kuwa Rais Kikwete alishiriki kuwabeba wawekezaji hao, hasa baada ya matatizo yaliyosababishwa na Richmond. Na blogu hii inajua kuwa Rais Kikwete anataka Dowans walipwe pesa zao, lakini anakosa ujasiri kwa sababu za kisiasa. SOMA Maswali Magumu hapa.

5 comments:

"Star" said...

Nikiwa muumini mzuri wa Maswali Magumu, ninaamini YOTE yaliyoandikwa kwenye makala hayo. Na JK asitudanganye; kauli na utetezi wake ni dhaifu, HATUDANGANYIKI!

"Star" said...

Nikiwa msomaji mzuri wa MASWALI MAGUMU, ninaamini YOTE yaliyoandikwa kwenye makala hayo. JK asitudanganye; kauli na utetezi wake ni dhaifu, HATUDANGANYIKI!

Anonymous said...

mimi naona kizungu zungu na jinsi yaha maisha yanavyozidi kuwa magumu vitu vinapanda kiholela hii yote ni kwa sababu ya uongozi mbovu. ss kama huyo mmiliki hajulikani kwa nn serikali isitaifishe hiyo mitambo? hawa viongozi wetu wapo kwa ajili ya maslahi yao tu tumewachagua watutetee ktk vitu kama hivi lakini kimya sijaona mmbunge akigoma kupokea posho kwa sababu ya jambo fulani. hao wote neio hao hao tu.

Anonymous said...

KIKWETE ni Dowans na Dowans ni Kikwete. Hawa wote mnaowaona wakijileta leta ni mawakala wake wanaodhamiria kumficha ili aendelee kuonekana wa maana wakati hana maana kabisa.

Anonymous said...

Mzee wa maswali magumu nina swali, je Lowasa ni waziri mkuu mstaafu? au ni waziri mkuu aliyejiuzulu?

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'