Sunday, November 19, 2006

Unasemaje juu ya vitisho vya Lowassa?


Waziri Mkuu, Edward Lowassa, amekuwa akitumia mabavu kukabiliana na wananchi wanaomkosoa, hasa magazetini. Makala HII imemuonya na kumtahadharisha juu ya athari za ubabe huo; hasa kwa mtu ambaye tayari ameshaonyesha nia ya kuwania urais baada ya Jakaya Kikwete. Una maoni gani?

3 comments:

Reggy's said...

Ndugu yangu nakupongeza kwa kushindwa kuwa miongini mwa wanaotishwa. Wewe si muoga, umechambua masuala mazito sana kwa ujasiri mkubwa sana. keep it up

Anonymous said...

Lowassa kiloriti hizo na mambo ya urais bado kitendawili sana,bongo sio ile ya zamani kwanza elimu yake na achivement?

Anonymous said...

Lowasa ameshindwa kuthibitisha kwamba aliteuliwa na JK kwa sababu ya uwezo wake na si uswahiba. Ameamua kuleta masikhara kwenye kazi. Masikhara si mabaya, lakini si kwa mtu wa kiwango cha PM na nchi kama Tanzania. Amekazania kufunikana tu.
Ni hatari kuwa na PM na Rais ambao wote ni watu wa platforms, wanapiga kampeni badala ya kuongoza.
Anawakemea Technocrats mbele ya wananchi ili awe safi. Nyingi za amri zake ni za kiimla na zisizo na busara.
Ameanza maandalizi mapema baada ya kuona media ilimbeba JK, Lakini mguu aliyoanzia ni mbaya.
Ataweza kuwanyamazisha wabunge wa CCM lakini sio watu makini wasio waoga wala wanafiki.
Nilishtushwa kuona analeta mipasho bungeni eti tumejaa tele! Naambiwa ana digrii ya Fine and Performing Art, kwa hiyo ilo ni suala la kawaida na alikuwa akikumbushia enzi.
Cha ajabu anaionea aibu digrii yake, tembelea tovuti ya Bunge uone wasifu wake..anajitambulisha kama mtu mwenye Masters.
Wana-Mtandao walijipanga kisayansi kuchukua nchi! Lakini ni majuha wa Kuongoza nchi kwani hawakuwa na MKAKATI wowote baada ya hapo!
Tumepata Rais wa misiba na safari kama Vasco Da Gama! Kazi kuuza sura tu!
Eti watanzania wanasubiria 2010! wameliwa, 2007 tu ni mbali

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'