Monday, January 15, 2007

JK mbona unataka kuwanyonga rafiki zako?


Rais Jakaya Kikwete amekuwa akijitambulisha na kutambulishwa kama 'rafiki' wa wanahabari. Ajabu ni kwamba serikali yake inataka kudhibiti habari kijanja, kuficha 'mambo'yake. Ndiyo maana imeshirikiana na baadhi ya wadau wa habari, kuandaa muswada wa utumwa wa habari kwa kisingizio cha kutunga sheria ya uhuru wa habari. Lakini hii siyo iliyokusudiwa na wadau. Juu juu muswada unafanana na uhuru; ndani ni utumwa mtupu. Mwenzetu mmoja, akiakisi sauti za wanaharakati wengi waliogundua janja ya serikali ya Kikwete kunyonga vyombo vya habari, huku yeye akitabasamu, nao wakifurahi, amekataa. Anasema: SITAKI. Hataki nini? Soma mwenyewe; toa maoni.

4 comments:

Anonymous said...

Wakibanwa wanasikiliza

soma: http://www.mwananchi.co.tz/mwananchisite/Mwananchi/Habari/Habari1.asp

Anonymous said...

inasomeka hivi:

Waziri, wanahabari wazidi kulumbana kwa muswada

Na Midraji Ibrahim

WAZIRI wa Habari, Utamaduni na Michezo, Muhammed Seif Khatib amesema haikuwa lazima kuwaita wadau wa sekta ya habari nchini wakati wa kuandaa rasimu ya muswada wa marekebisho wa sheria ya vyombo vya habari.

Akizungumza katika Ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam jana, Waziri Khatib alisema hivi sasa ndio wakati muafaka kwa wadau hao kushirikishwa.

Kauli hiyo inatokana na kuwepo malalamiko kuwa walioshiriki kuandaa muswada huo, hawakutoka taasisi za vyombo vya habari.

Khatib alisema wanasubiri kupata mapendekezo ya muswada huo kutoka kwa wadau hao ambao alisema wameahidi kuyapeleka mwisho mwa mwezi huu, huku akisisitiza kuwa hawana haki ya kukataa muswada.

"Hawana mamlaka ya kukataa, bali kusema tunataka iwe hivi. Wenye mamlaka ya kukataa muswada ni wabunge kwa sababu ndio wawakilishi wa wananchi," alisema.

Kuhusu kubebeshwa lawama na wadau, Waziri Khatib alisema ni halali kwa sababu yeye (Khatib) anamwakilishi Rais katika kuongoza sekta hiyo.

Muswada huo umepata upinzani kutoka kwa wadau, wakidai kuwa unazuia uhuru wa vyombo vya habari na utakuwa kikwazo dhidi ya vita ya kupambana na rushwa na kwamba iwapo utapitishwa utawanyima wananchi kujua masuala yanayofanywa na serikali.

Tayari Baraza la Habari Tanzania (MCT), limeanza kuandaa rasimu mbadala ya muswada huo jinsi wanavyotaka uwe kwa ajili ya kuwasilisha kwa Waziri Khatib.

Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (Moat), kimekanusha kuhusika na kukataa muswada huo, na kusema kuwa kilishirikishwa kwenye semina za kujadili muswada huo ambao umekataliwa na asasi nyingi.

Mwenyekiti wa Moat, Reginald Mengi alisema wadau wa sekta ya habari wanaamini watafanikiwa kwenye mapambano ya kusimamisha muswada huo kwa sababu, Rais Jakaya Kikwete ni msikuvu anayepanda uhuru wa kujieleza.

Anonymous said...

Miswada ya sheria kutafsiriwa kwa Kiswahili

Na Simon Berege, Dodoma

WIZARA ya Sheria na Mambo ya Katiba inaangalia uwezekano wa kuitafsiri kwa lugha ya Kiswahili miswaada yote ya sheria inayowasilishwa bungeni, ili kuongeza uelewa wa miswada hiyo ambayo kwa sasa inaandaliwa kwa lugha ya Kingereza.

Akijibu awali la Mbunge wa Rahaleo, Saleh Farrah, Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Dk Mary Nagu, bungeni jana, alisema pamoja na miswaada hiyo, wizara yake inakusudia kuzitafsiri sheria mbalimbali kuwa katika lugha ya Kiswahili baada ya kuimarika
kwa kitengo cha tafsiri kilicho katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mbunge huyo alitaka kujua kama Serikali iko tayari kutafsiri miswaada yote ya sheria inayofikishwa bungeni, ili kuongeza uelewa kwa miswaada hiyo na kuondoa utata unaoweza kujitokeza kutokana na miswaada hiyo kuwa katika ligha ya Kingereza.

Waziri Nagu alisema sheria kadhaa tayari zimeshatafsiriwa kwa Kiswahili, ikiwemo ya Ardhi ya vijiji, sura 144, Sheria ya Ndoa, sura ya 29, Sheria ya mabaraza ya kata, sura ya 206 na Sheria ya Filamu na Michezo ya Jukwaani sura 230 na kwamba sheria kadhaa zipo katika hatua ya mwisho kutafsiriwa ikiwemo ya Mazingira ya mwaka 2004.

“Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, lugha inayotumiwa kuandika sheria siyo lugha nyepesi, ni lugha ya kitaalam, hivyo hata sheria zikiandikwa kwa Kiswahili bado maudhui yake yanaweza yasieleweke kwa wananchi, iwapo hakutakuwa na juhudi za ziada za kutengeneza vijarida au vipeperushi kwa ajili kufafanua maudhui ya sheria hizo,” alfahamisha Dk.
Nagu.

Naye Mbunge wa Ukerewe, Getrude Mongela, alisema kuna umuhimu wa kutiliwa mkazo
suala la kutafsiri sheria hizo, kwani katika maeneo mbalimbali duniani, ikiwemo vikao vya Bunge la Afrika Kiswahili kimekuwa kikitumika kama lugha rasmi ya mawasiliano.

Mongela ambaye pia ni Rais wa Bunge la Afrika alisema katika kurahisisha kazi hiyo serikali inaweza kuwatumia vijana wanaoweza kufanya kazi hiyo, ambao hawana ajira kwa sasa, ambapo Waziri Nagu, alisema serikali itauzingatia ushauri huo kulingana na uwezo wa bajeti yake.

Mwananchi 7.2.2007

Anonymous said...

asilete unajanja na kwanza, aanze mikakati ya 2008 bila kujidai, kwani nchi yake itaendelea kuwa mskini, bora aache tabia ya kuumiza baadhi ya watu vichwa kijanja jana, anajijua mwenyewe, anayotenda rohoni kwake, wengine ujumbe unafika, usijifanye mwema ukisaifiri nchi za watu, wakati, una chuki na baadhi ya watu, toa chuki zako hizo haraka sana. iga mfano wa maraisi wa nchi zingine, be careful

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'