Saturday, August 18, 2007

Kishindo cha Zitto Kabwe


Dar es Salaam inazizima. Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amegeuka shujaa wa mwaka. Habari kutoka Dar zinasema amekuwa gumzo kila kona, wala mvua nzito haikuweza kuwazuia wananchi kuandamana na kusukuma gari lake kutoka Ubungo hadi viwanja vya Jangwani, Jumamosi, Agosti 18, 2007, alikohutubia mkutano mkubwa na kusema Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, alisaini mkataba katika Hoteli ya Churchill, London, Uingereza.

Watawala wameduwaa. Bomu walilompasulia Zitto kumdhalilisha limewalipukia wenyewe! Hiki ndicho kishindo kinachozungumzwa. Anasema "tusikumbatie walioshiba" Ipate pia kwa kimombo Hoja kamili na mjadala wake Bungeni HII HAPA. Baadaye, wawekezaji wenyewe, Barrick walijitokeza kutoa maelezo HAYA, lakini Zitto akayachambua pia maelezo hayo na kubainisha uhusiano wa karibu sana kati ya waziri na wawekezaji, huku wakitoa maelezo yanayojikanganya zaidi.

3 comments:

Anonymous said...

Watanzania naomba tuamke, tunayo vita kubwa mbele yetu,lakini bahati mbaya hatumjui adui tunayepigana naye!!!!
Vita iliyopo ni baina ya TABAKA KONGWE dhidi ya TABAKA JIPYA.

Tabaka kongwe linajumuisha wazee wengi walio na madaraka serikalini na kwenye chama cha mapinduzi,maamuzi mengi wanayofanya ni kuhakikisha uwepo wao kwa sasa na siku zijazo mfano,kutotofautisha maana ya utumishi wa umma,yaani mstaafu serikalini anahamia kuwa mbunge tena bila kikomo,takrima kwenye uchaguzi,kukataa wagombea binafsi, mpango haramu kuuziana nyumba za serikali nyigi zikiwa kwenye maeneo mazuri, kuongeza muda wa kustaafu,kuingia ubia na makampuni ya nje kuvuna rasilimali za nchi,kukataa bunge lisiweke kikomo cha kuwa mbunge,kuunda vyombo vya kulinda wala ji na watoaji rushwa,nk.

Tabaka jipya ni la vijana wa nchi hii wenye uchungu halisi na mustakabali wa maisha ya watanzania.

Lazima tujue kwamba CCM ni adui wa pili, wa kwanza ni hawa wazee!!!

Lazima tujue pia kuwa vijana wa kitanzania inatilazimu tuingie kwenye siasa sasa!!!!

Tukiweza kuwakataa kupitia sanduku la kura!!! hawatakuwa na nguvu nyingine tena. tutakuwa tumewamaliza!!!

Tunachopaswa kufanya ni kujenga uelewa miongoni mwetu vijana kumtambua adui yetu ni nani hasa kata ya CCM na hawa viongozi wazee!!!tuvitumie vizuri vyombo vya habari,tuache mizaha na udaku,huu si muda wa kufanya hayo!!!

Tukilielewa hilo wote pamoja vita tutaimaliza haraka iwezekanavyo na kukamata kasi ya maendeleo kama mataifa mengine.

Anonymous said...

Hapo umenena mwanangu. Vijana tuamke, tuache kuchezeshwa mdundiko na Komba. Elimu yetu inapota bure kama hatuwezi kujipigania!

Siriha said...

Tatizo sio kati ya vijana na wazee bali ni kati ya mawazo endelevu na mawazo mgando; hivi havinauhusiano na umri wa mtu!! Hawa wanaohujumu uchumi wetu KARAMAGI,MALIMA na wanamtandao maslahi wenzao si ndio hao wanajiita vijana? Kuikomboa nchi yetu twahitaji wazee na vijana wote kwa pamoja wenye uchungu na Tanzania na wenye fikra sahihi!!!!

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'