Tuesday, January 29, 2008

Kofi Anna bado amekwama Kenya

Ufumbuzi wa mgogoro Kenya bado ni mgumu. Mauaji yanaendelea, huku Mwai Kibaki na Raila Odinga hawajakubaliana mahali pa kuanzia mazungumzo, bado wanashitakiana kwa mauaji ya kimbari. Na kwa mara ya kwanza, mwansiasa, mbunge wa upinzani kauawa na kuibua ghasia mpya. Wakati huo huo, jamii inaendela kumshinikiza Kibaki ajitoe mhanga kuleta amani. Sasa Kofi Annan na timu yake ya wapatanishi wametoa ajenda ya mjadala wa usuluhishi. Itakubalika sawa kwa pande zote?

Friday, January 25, 2008

Tabasamu hili linaficha nini?


Kenyan embattled President Mwai Kibaki shakes hands with ODM leader Mr Raila Odinga at Harambee House, Nairobi, on Thursday. Picture by Govedi Asutsa. Source: The Standard Online, January 25, 2008. But mistrust still reigns. See here: 00. 01. 02. 03 04. 05. 06. 07. 08. 09. 10.

Tuesday, January 22, 2008

Raila ampeleka Kibaki kizimbani

Ukisikia Nguvu ya Umma ndiyo hii. Matukio haya yanaendelea kudhihirisha kwamba sasa Kenya inaongozwa na marais wawili. Mmoja wa kuchaguliwa na wananchi na mwingine wa kupachikwa na Tume ya Uchaguzi. Mmoja anashikilia na kutumia vyombo vya dola, mwingine anashikilia na kutumia imani ya wananchi. Acha Kibaki akae Ikulu, lakini kama analala usingizi, basi si binadamu mwenzetu. Moto bado unawaka, na kama mambo yataendelea hivi, na hasa baada ya ODM kumfikisha kizimbani, cha moto atazidi kukiona. Soma mwenyewe.

Wakati huo huo, mambo yanaanza kupata mwelekeo nchini Kenya baada ya Kofi Anna kuanza kazi ya usuluhishi na upatanishi. Baadhi ya mapya mpya haya hapa. 0. 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10.

Sunday, January 20, 2008

CCM ya ufisadi na utumwa

Msanii huyu wamemnunua, wakampa ajira na uanachama, na wakamuahidi makubwa, halafu wakamnyima. Sasa ameamua kubwaga manyanga na kuwarudishia kadi yao. Nionavyo mimi, kununua na kuchuuza binadamu wenzetu ni ufisadi na ni utumwa unaoendekezwa na CCM ya Jakaya Kikwete na Yusuph Makamba. Soma na toa maoni yako.

Friday, January 11, 2008

Hongera Dk. Slaa


Kwamba Rais Jakaya Kikwete amemfukuza kazi Gavana wa Benki, Daudi Ballali, ni jambo la kutia moyo. Pongezi anazopata Rais Kikwete sasa anazistahili. Lakini sote tunajua kwamba Rais Kikwete amelazimika kuchukua hatua hizo, ingawa serikali ilikuwa inajua 'matatizo' ya Benki Kuu. Kama si Dk. Willibord Slaa (pichani) na wenzake kuibua hoja hiyo Bungeni na kushinikiza serikali ichukue hatua, uchunguzi usingefanyika, na hatua hii moja isingechukuliwa. Kwa sababu hiyo, wanaompongeza Rais Kikwete wasimsahau yule aliyemsukuma, Dk. Slaa.
Haya yote yameonyesha kuwa serikali na watu wake ilijua ukweli wa tuhuma alizotoa Dk. Slaa, ndiyo maana hata Jaji Mark Bomani akawaonya waliotishia kumshitaki mtoa tuhuma, ambao waliishia kutoa vitisho lakini hadi leo hawajakanyaga mahakamani. Na sasa tayari ametangaza kuwa ana siri nyingine kubwa za wizi wa vigogo. Ndiyo maana nasema, katika hili la JK kuchukua hatua, shujaa ni Dk. Slaa. Na tayari kuna dalili kwamba Ballali hatakubali kutolewa kafara na kufa peke yake.
Tetesi zinazovuma sasa, kutokana na usiri wa serikali juu ya suala la Ballali, ni kwamba ugonjwa wake ulisababishwa na sumu aliyolishwa kumkolimba, ili siri zao zisitobolewe! Lakini sasa inasemekana naye kaamua kufa na serikali.

Tuesday, January 08, 2008

Asanteni

Kwa unyenyekevu mkubwa, nawashukuru walionipendeza kwa tuzo hii ya Excellence in ICT Journalism katika Afrika. Siwajui, wanajijua. Nawashukuru na majaji walionipigia kura. Asanteni!

Sunday, January 06, 2008

Wahariri wakatwa mapanga

Wapambanaji wenzetu wawili, Ndimara Tegambwage na Saed Kubenea, wanaochapisha gazeti la MwanaHalisi wamevamiwa ofisini na kukatwa mapanga Jumamosi 6, 2008 katika ofisi za gazeti hilo, Kinondoni, Dar es Salaam. Tayari hisia za wananchi zinawatuhumu baadhi ya mafisadi serikalini na wapambe wao, kwa kuandaa 'ujambazi huu.'

Kubenea ndiye Mhariri Mtendaji na mmiliki wa gazeti hilo, wakati Ndimara ni Mhariri Mshauri na 'mashine' ya kitaaluma ya gazeti hilo.

Gazeti hilo limekuwa na makala na habari kali mno dhidi ya wezi ndani ya serikali. Mara kadhaa Kubenea ameonywa na Ofisi ya Waziri Mkuu na Idara ya Habari (MAELEZO) kwa barua, simu na mdomo. Kuna wakati gazeti 'lilivamiwa' na watendaji wa serikali kwa kisingizio cha kukagua 'uwezo wa kitaaluma wa waandishi' wa gazeti hilo. Mara nyingine lilivamiwa na watu wa TRA, eti kutazama kama linaipa kodi.

Vile vile, ndilo hazeti lililowahi kumtuhumu kiongozi mmoja wa juu serikalini, ambaye lilimuita Bwana 'mvi' kwa kuwaagiza wahariri kadhaa rafiki zake waanze mkakati wa kuwaandama wakosoaji wa serikali.

Ikumbukwe kwamba ndilo gazeti pekee lililotaja majina ya mafisadi waliotajwa na Dk. Willibroad Slaa bila kificho, mbele ya umma, pale Mwembe Yanga, Dar es Salaam.

Tujadiliane


Mwaka 1991, aliyekuwa Rais wa Zambia, Kenneth Kaunda alishindwa na wapinzani katika uchaguzi mkuu, akawakabidhi madaraka bila ghasia. Mwaka 2000, aliyekuwa Rais wa Senegal Abdou Diouf alikabidhi madaraka kwa washindi na kuondoka Ikulu kwa amani. Mwaka 2002, aliyekuwa Rais wa Kenya, Daniel arap Moi, alimkabidhi Mwai Kibaki (pichani kushoto) uongozi, baada ya mteule wake aliyeandaliwa kuwa mrithi wake, Uhuru Kenyatta wa KANU, kushindwa na nguvu ya upinzani.

Mwai Kibaki aliyepishwa na Moi, ameshindwa kukubali matokeo baada ya miaka mitano tu ya kukaa Ikulu na kukataliwa na wapiga kura. Ghasia zimezuka, damu zimemwagika. Amejiunga na klabu ya marais wezi wa kura, kina Robert Mugabe na Amani Karume. Tanzania tunajifunza nini? Afrika yetu inaelekea wapi? Tufanye nini kuinusuru? Hawa wametoa maoni yao. Wewe una maoni gani? Tujadiliane.


My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'