Sunday, January 06, 2008

Wahariri wakatwa mapanga

Wapambanaji wenzetu wawili, Ndimara Tegambwage na Saed Kubenea, wanaochapisha gazeti la MwanaHalisi wamevamiwa ofisini na kukatwa mapanga Jumamosi 6, 2008 katika ofisi za gazeti hilo, Kinondoni, Dar es Salaam. Tayari hisia za wananchi zinawatuhumu baadhi ya mafisadi serikalini na wapambe wao, kwa kuandaa 'ujambazi huu.'

Kubenea ndiye Mhariri Mtendaji na mmiliki wa gazeti hilo, wakati Ndimara ni Mhariri Mshauri na 'mashine' ya kitaaluma ya gazeti hilo.

Gazeti hilo limekuwa na makala na habari kali mno dhidi ya wezi ndani ya serikali. Mara kadhaa Kubenea ameonywa na Ofisi ya Waziri Mkuu na Idara ya Habari (MAELEZO) kwa barua, simu na mdomo. Kuna wakati gazeti 'lilivamiwa' na watendaji wa serikali kwa kisingizio cha kukagua 'uwezo wa kitaaluma wa waandishi' wa gazeti hilo. Mara nyingine lilivamiwa na watu wa TRA, eti kutazama kama linaipa kodi.

Vile vile, ndilo hazeti lililowahi kumtuhumu kiongozi mmoja wa juu serikalini, ambaye lilimuita Bwana 'mvi' kwa kuwaagiza wahariri kadhaa rafiki zake waanze mkakati wa kuwaandama wakosoaji wa serikali.

Ikumbukwe kwamba ndilo gazeti pekee lililotaja majina ya mafisadi waliotajwa na Dk. Willibroad Slaa bila kificho, mbele ya umma, pale Mwembe Yanga, Dar es Salaam.

6 comments:

Anonymous said...

Ufisadi kama huu nao utokomozwe mara moja kama ndio hivyo sifikirii kama ndio ni watu wa kawaida sidhani hivyo basi kuna kila dalili za maharamia kuvamia na kutumwa na watu maalumu wanajulikana, maana kama ndio hivyo basi kuna haja ya kuangalia mpya nani amefanya haya mambo ya ajabu sana,
John Massawe

James said...

Tukishasema hii serikali ya wahuni, lakini bado kuna watu wanaitetea. Tutaona mengi mwaka huu. Poleni mlioumizwa.

Anonymous said...

Kumbuka wakati ukiandika na kuwaonya watu na waandishi makini, Sifikirii kusema ni watu wa kawaida maana hao wanahitaji kutetewa na watu na waandishi makini, Siyo watu bali ni mafia na genge la wahuni na mtindo mpya, utaona mengi sana kadri ya siku zinavyoweza kwenda mbele, Pengine watu maharamia wengine wanaogopa, kama ndio hivyo basi kuna mikakati mingine ya waandishi wengine makini.
Josh Michael

Salum said...

Hawa ni wahuni wale wale tu, taifa linawajua, na watapatikana tu. Wasijidai kwamba pea na madaraka yao vitawaaidia.

Samson said...

Poleni mlioumizwa na 'mafisadi.' Yan mwisho hayo...alisema yule jama kwenye KULI (nani vile? Chonya, sio?)

Anonymous said...

Poleni sana waandishi kwa kukutwa na kile kilichoitwa "ajali kazini". Hii si ajali bali ni jinai. Ili mufanye kazi kwa tahadhari itakuwa vema endapo mtaweka kamera za siri za ulinzi katika maofisi yenu. Najua hii haitamaliza matatizo ya kushambuliwa, kwani hasidi haachi kujaribu, italeta hofu kwa majambazi ' vilaza'. Pengine ndicho rais alikimaanisha kuhusu kuchukua tahadhali. Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi, na hakika mliobaki hamtardusha majeshi nyuma. hii ni dalili ya ushindi.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'