Friday, January 11, 2008

Hongera Dk. Slaa


Kwamba Rais Jakaya Kikwete amemfukuza kazi Gavana wa Benki, Daudi Ballali, ni jambo la kutia moyo. Pongezi anazopata Rais Kikwete sasa anazistahili. Lakini sote tunajua kwamba Rais Kikwete amelazimika kuchukua hatua hizo, ingawa serikali ilikuwa inajua 'matatizo' ya Benki Kuu. Kama si Dk. Willibord Slaa (pichani) na wenzake kuibua hoja hiyo Bungeni na kushinikiza serikali ichukue hatua, uchunguzi usingefanyika, na hatua hii moja isingechukuliwa. Kwa sababu hiyo, wanaompongeza Rais Kikwete wasimsahau yule aliyemsukuma, Dk. Slaa.
Haya yote yameonyesha kuwa serikali na watu wake ilijua ukweli wa tuhuma alizotoa Dk. Slaa, ndiyo maana hata Jaji Mark Bomani akawaonya waliotishia kumshitaki mtoa tuhuma, ambao waliishia kutoa vitisho lakini hadi leo hawajakanyaga mahakamani. Na sasa tayari ametangaza kuwa ana siri nyingine kubwa za wizi wa vigogo. Ndiyo maana nasema, katika hili la JK kuchukua hatua, shujaa ni Dk. Slaa. Na tayari kuna dalili kwamba Ballali hatakubali kutolewa kafara na kufa peke yake.
Tetesi zinazovuma sasa, kutokana na usiri wa serikali juu ya suala la Ballali, ni kwamba ugonjwa wake ulisababishwa na sumu aliyolishwa kumkolimba, ili siri zao zisitobolewe! Lakini sasa inasemekana naye kaamua kufa na serikali.

8 comments:

Anonymous said...

Huyu ndio mtu wa kumpa HONGERA SANA SANA SANA kwa kazi nzuri sana aliyoifanya na hivyo wakati mwingine Wabunge wa CCM waache kushabikia siasa kama vile wao ni watu na serikali, Hivyo kuna haja sana ya kuwa na wabunge kama waha kama 50 hivi nchi ingenyooka na kuwa na nidhamu sana, Then Ndugu yangu ngurumo lazima tupongeze vyombo huru vya Habari kwa kazi nzuri vilivyofanya na kuona kuwa wanandika bila ya woga, then Kama Rais angefuta Ushauri wa Professor Lipumba kipinndi fulani kuwa amshauri mtu mzuri nani leo mambo yasingekuwa hivi, je hapa nani aliyefanya kazi, Hongera Slaa kwa kazi nzuri sana.
Josh Michael
colorado

Anonymous said...

Ukiona kuwa mlolongo wa firms hizo ni wakati wa 2005 kwanini kipindi hicho??sasa kuna tuhuma nyingi sana sana serikali yetu ilikebishe haraka na kufanya kweli wote ni watanzania
Josh

Anonymous said...

Fisadi kikwete anapewa hongera za nini? Wakati yeye ni mwizi mmojapo. Ama kweli Watanzania tuna safari ndefu ya kujikomboa.

Ee Mungu tunusuru sisi viumbe wako.

Anonymous said...

Pongezi kwa serikali ni mbaya sana tena hiyo hiyo iliyosimamia ufisadi wa kutisha kama huo ni hatari sana, kama kweli watu wetu ni wazuri na idara husika iweje waruhusu makampuni haya yote yachukue fedha za watu maskini, Je kuna kila haia Gavana ni kichwa tu kuna idara, na idara za serikali zote na kuidhinisha fesha zote hizo, Je hivyo kama kweli hizo zingetumika katika kujenga shule leo tungekuwa wapi?? Hivyo vyombo vya rushwa vilikuwa wapi?? je kuna maswali kama 1000 hivi hapa, sijui sisi tutakuwa lini watu na waaminifu katika hili. Je Hata idara nyingi sana katika malipo haya, Jamani ndugu zangu walio katika madaraka sasa yatosha kuiba jamni achane ili maskini wapate huduma bora za afya, Mungu lazima waape adhabu kwa kuwaibia maskini kama hivi.
Josh Michael

katibu said...

Hongera Mbunge wetu, mtetezi wa wanyonge, Dk Slaa. Tuko nyuma yako.

Bobby said...

JK ameipa kazi bodi iliyoshindwa kazi na kumwacha balali na wenzie wafanye watakavyo eti ifanye uchunguzi then ichukue hatua. Jamani mbona haya ni maigizo ya ajabu kabisa yanafanywa na rais wa nchi. Kimanagement gavana akituhumiwa kwa ubadhilifu kwa kiwango kile maana yake bodi ya BOT mpaka waziri wa fedha nao wanapaswa wajiuzuru au wafukuzwe kazi lakini haya ya TZ ni utumbo uliokosa maelezo.

Mm sielewi kama nchi tunaelekea wapi kwa style ya viongozi hawa tulionao.

Mungu ibariki Afrika Mungu, ibariki Tanzania.

Anonymous said...

Leo hii tunapo fikiria hatima ya ufisadi wa BoT, yapi atakayokujanayo Billali huko alipo, taifa na umma kwa ujumla yatupasa kumkumbuka Mbunge wa karatu, Dr. Slaa, mcahngo wake mkubwa alioutoa kwa serikali, japo serikali bado hau appriciate tunaamini ipo siku watakuja kukubaliana na ukweli.
Changamoto inayotolewa na upinzani inaleta 'accountability to the government officials" kwahiyo mchango wao unatakiwa kuthaminiwa.
Watanzania tuungane kuikomboa nchi yetu katika dimbwa la ufisa.
Mansweat, Iringa

bulesi said...

Haya yote anayofanya Kikwete kuunda tume kuchunguza makampuni yaliyochota fedha BOT ni kiini macho na danganya toto tu kwasababu Kikwete anafahamu ufisadi wote huu na fedha zilikokwenda na ndio maana akamteua Meghji kuwa mbunge halafu waziri wa fedha kwa kujua angemtumia kuchota fedha bila wasiwasi kupitia kampuni za maswahiba wake. Msiwafanye watanzania wajinga!!! Zakia anajua kuwa Rostam alikuwa anakwenda ofisini kwake kila jumatatu asubuhi na fedha zilikuwazinachotwa. Sasa nani atamgusa Rostam Aziz?

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'