Sunday, January 20, 2008

CCM ya ufisadi na utumwa

Msanii huyu wamemnunua, wakampa ajira na uanachama, na wakamuahidi makubwa, halafu wakamnyima. Sasa ameamua kubwaga manyanga na kuwarudishia kadi yao. Nionavyo mimi, kununua na kuchuuza binadamu wenzetu ni ufisadi na ni utumwa unaoendekezwa na CCM ya Jakaya Kikwete na Yusuph Makamba. Soma na toa maoni yako.

6 comments:

Fweda said...

Huwa navutiwa sana na makala zako mkuu,mie kwa sasa sina chama lakini nataka kuwa mwanachama wa chama cha siasa lakini sio ccm sijui ndg yangu unanishauri nijiunge na chama kipi?Kwa mtazamo wako unachoona kitanifaa?!Najua katika majibu yako utanijibu kujiunga chama ni hiari ya mtu kikatiba,mie ningependa sana wewe unishauri kwa kuwa ni mchambuzi mzuri wa vyama vya siasa,nimesoma makala zako nyingi umesha nitosheleza na ya kuwa CCM haifai mafisadi hilo halina mjadala.
Sasa tunaomna utueleze chama kitacho nifaa kuwa mmfuasi wake.Tafadahali naomba unishauri kwa kutaja chama kimoja.Ahsante

Jared said...

CCM wamezidi kununua watu kwa sababu hawawezi kuwashawishi wawaunge mkono. Ufisadi wa Tanzania unakuzwa na kupenda pesa kuliko utu, na kama CCM wananunua watu ni moja kwa moja wanadhalilisha utu wa Watanzania wenzao, kwa vile tu wana pesa ya kutoa na kuwalaghai! Kama alivyosema Ngurumo, huu ni utumwa...tuukatae.

masa said...

huyo bwana aneomba ashauriwe ajiunge na chama gani,,,kwa'ruksa ya ngurumo naomba nimjibu,,,kama kweli sio ccm namshauri aende mashuleni,wodini mahospitalini, barabara vijijini, urasimu maofisini, waajiriwa walivopewa sehemu nyeti kw kujuana, viongozi wasivopenda kuwa waadilifu kw umma ....bwana huyu atapata jibu ajiunge na chama gani, ni uwongo usioepukwa na wakubwa na ndugu zao kwamba wene dhamana hawajui shida zinazowasibu wananchi wa kawaida hasa watoto, wakina mama, wasiojiweza,,,lakini wao wameweka full (AC) kweny MVX yao naamin siasa za kenya zinaelekea kwetu, utajua sasa ujiunge na chama gani. karibu sana

Anonymous said...

unasubiri ruhusa ya ngurumo kujiunga na chama cha siasa? hiyo haki yako bwana, au sio?

Ansbert Ngurumo said...

Ndugu yangu FWEDA,

Asante kwa salaam. Nimeliona ombi lako. Si jepesi. Binafsi sina chama cha siasa. Lakini navitazama na kuvichunguza vyote vilivyopo. Nasoma majira na alama za nyakati. Natafakari na kuichunguza historia. Ndiyo maana nimefika mahali nikashawishika kwamba CCM imemaliza ngwe yake. Hata tukiilazimisha kuendelea, hakun ajipya linalotarajiwa kutoka huko.

Sasa hiyo ilikuwa hatua ya awali ya kutambua tatizo. Ya pili, ni kutafuta tiba. Na hapo ndipo mimi na wewe tulipo sasa. Tunawatazama hawa waliopo nakusema, "yupi apewe dhamana? Yupi aungwe mkono? Yupi asaidiwe? Yupi anaweza kupokea mawazo mapya akayakubali na kuyatumia bila jeuri na majivuno ya uzoefu? Yupi anstahili kuongezea nguvum kujengwa na kuimarishwa ili wakati ukifika awe tayari na imara? "

Hiyo ndiyo changamoto tuliyo nayo. Kwa kuwa hii si hesabu, hatuwezi kusema jibu ni kadha wa kadha. Lakini lipo. Kazi yetu ni kulitafuta. Naamini tutaipata kwa kulitafuta, si kwa kuletewa na mtu yeyote.

Zaidi ya hayo, si lazima kila Mtanzania awe mwanachama wa chama cha siasa. Siasa zinatuhusu. Hatuwezi kuzipuuza. Lakini tunaweza kuzifanyia kazi (kuziunga mkono) bila kuwa wanachama. Ni haki na jukumu la kila mmoja kuwa pale anapodhani panamfaa zaidi.

Anonymous said...

Chama au si uanachama vyote vyatawaliwa na wajeuri.
Angalia tunapokopi udemokrasia- waniba kura na mambo mengine machafu.
Kumbuka kaka wataalamu wa dunia hii ni hatari. Utadhani kuwa ubadhilifu na ufisadi wote uko hapo tza tu, lakini ukweli ni kwamba umeenea kote. Waenezao haya ni wachache tu duniani. Na haya yalianza zamani.
Ingia website hizi uone.
http://judicial-inc.biz/slave_traders_.htm,
http://judicial-inc.biz/b.lood_diamonds.htm,
http://judicial-inc.biz/J_oran_va_der_sloot_supplement.htm,
http://judicial-inc.biz/thersea_heinz_kerry_bio.htm,
http://judicial-inc.biz/1.osephardim_of_curacao.htm,
http://judicial-inc.biz/j_history_caribbean_jews.htm,
http://www.blacksandjews.com/Jews.of.Black.Holocaust.ag.html,
http://sunray22b.net/slavery.htm,
www.jewwatch.com, www.erichufschmid.net, www.iamthewitness.com, www.prothink.org.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'