Saturday, January 31, 2009

Chozi la Pinda


Baada ya yote yaliyoandikwa na kusemwa, kuhusu kauli ya kuomba radhi na chozi la Waziri Mkuu Mizengo Pinda (pichani juu) akiwa Bungeni wiki hii, bado najiuliza: Amewalilia albino au serikali, au amejililia yeye? Au kuna jambo jingine lililomliza? Kwa kuwa alipotoa kauli tata tulisema ni kauli ya serikali, je kilio hiki cha waziri mkuu ni kilio cha serikali? TUJADILIANE.

4 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Ni ngumu saana kupata jibu la wazi kama hawa watendaji huwa wanaiwakilisha serikali. Maana matendo na hata kauli zao wakati mwingine huwa haziendani ama kuonesha kutimiza matakwa ya serikali. Na wakati mwingine hata viongozi wanaonekana kukana kauli za wenzao waliozitoa. Kwa hakika alikuwa ziarani, alikwenda kama waziri mkuu na alitoa kauli kama waziri, kwa hiyo kihalali ingestahili kuwa kauli ya serikali. Lakini sidhani kama aliwasiliana na uongozi wowote ama washauri na waandika hotuba wa ofisi yake (kama anao) kuona ama kuhakikisha kuwa kila asemalo ni kwa maslahi ya Serikali. Tatizo ni kwamba viongozi wetu wana dhamana lakini hawaongozwi na dhamana hizo. Kama kuna kitu ambacho Waziri Mkuu anatakiwa kukitambua ni kwamba kuna kauli chache ambazo zikienda pande zote zamaanisha na kuboresha ile ya awali. Na moja wapo ni kwamba NI MUHIMU KUWA NA KAULI MAKINI NA SAHIHI lakini pia anatakiwa KUWA NA KAULI MAKINI NA MAKINI NI MUHIMU.

Anonymous said...

Pinda na Kikwete wote wasanii tu, ingawaje Pinda hajajizungushia wigo wa wezi.

Ansbert Ngurumo said...

Ndugu wapenzi wa Maswali Magumu na blogu hii,

Nawawekea hii ili kukuza mjadala. Msomaji mwenzenu ambaye hakujitambulisha jina, kutoka Bongo, alinitumia ujumbe wa maandishi kwenye simu. Tukajibizana. Ilikwenda hivi:

YEYE: Haukutaka kuumiza kichwa chako kwa kutoa mawazo mbadala kwa tatizo linalowakabili maalbino. Badala yake umekuwa mnafiki wa kisiasa kwa kuonyesha*****(ikakatika).

MIMI: Ndugu, umechelewa, lakini utaelewa taratibu kwamba najadili matendo na matamko ya kisiasa, ya wanasiasa, ktk mazingira ya kisiasa; na kwamba hata ujumbe wako kwangu ni wa kisiasa! Pili, si KAZI yangu kufikiri na kuandika kwa NIABA ya watawala, bali wananchi. Tatu, serikali makini haifanyi siasa ktk uhai wa watu. NGURUMO

YEYE akajibu: Brother,sijachelewa kwa kiwango cha kutojua upotofu wa mawazo yako! Ww inaonyesha ni bingwa sana wa kuakisi mawazo ya watu na ni mvivu sana wa kuumiza kichwa ili kufikiri na kutoa mawazo mbadala! Ikiwa unaandika mawazo ya wananchi ungetoa wazo la kusolve tatizo na si kuonyesha upinzani kwenye tatizo la kijamii kama hili.inaonyesha siasa imekukaa sana mawazoni mwako hasa siasa za kishari si siasa za kimapinduzi.unataka kujiigiza kuwa naturalist lkn haufanani! Ungefanana tuu kama ungetoa wazo mbadala kwa kuonyesha nn hakijafanyika mpaka ss either na serikali au hakuna wazo lolote lililotolewa na watanzania milioni 35.ww ulie msomi zaidi wa hull university toa wazo ambalo kwa ss watanzania litakuwa geni na lenye mafanikio ni si blabla za kusibiri wanasiasa waseme nawe upate uwanja wa kujijulisha na kuweka sura nzuri kwenye gazeti yenye mawazo potofu! Udsm Prf.@

MIMI nikajibu: Ndugu msomi! Tujenge hoja, tujibu maswali. Tufikiri, tutafakari. Tuchokoze na kuchokonoa. Tuchunguze, tuhoji na kufikirisha. Tutapata majibu mazuri NDANI YA VICHWA VYAO, bora kuliko litania ya mapendekezo. Kama huwezi kuumiza kichwa chako, umiza cha wengine. Yangu ni MASWALI, si MAPENDEKEZO! Yako ni yapi? NGURUMO.

...Baada ya hapo hajajibu tena. Wasomaji wengine mliosoma na kutafakari makala hii mna maoni gani?

MARKUS MPANGALA said...

DAIMA: nitakuwa mkweli na nitasimama katika ukweli kwamba chozi la Pinda haliakisi chochote katika suala la albino.
SABABU; nimejaribu kuitazama awamu ya 4 hadi nashangazwa na muundo wao kiuongozi,kimamlaka,kisera, n.k
LAKINI linalonishangaza ni kwamba kwanini serikali hii imejaa mzaha kiasi hiki? Kwanini serikali hii imekuwa kama watoto wadogo?
Ni kweli kwamba Pinda alitakiwa kulia kwa niaba ya albino au alilia baada ya kuona alitamka sicho?
Nilikuwa MBEYA wakati tukio likitokea, safari yangu ilikuwa kwenda Malawi kwa washkaji zangu, lakini nilitumiwa ujumbe kwamba Pinda analia, shauri ya kauli! ujinga gani huu tena uongozini?

TURUDI katika makala yako:
Mkuu umeuliza maswali, kwa kiasi ambacho mwenye akili anajua kwamba tunachokoza,tunafikiri lakini haya tunayofikiri yanatokana na matendo yao. Je tutakuwa na maswali iwapo wataenenda yale yanayohitajika? NB: kama kuna kitu ninakichukia katika level yangu hii ni kutaka kutumia nadharia ya fulani kuhukumu jambo fulani.
Vema tukatumia kauli au tamko kama ulivyoonyesha kuliko kutaka kutatua tatizo bila kuangalia nani amepewa mamlaka ya kutatua.

Msomaji uliyejibishana naye, simhukumu lakini ningetumia mtindo wangu wa siku zote kuuliza maswali kabla sijatoa maoni yangu kwake.
Kwa mfano ninaweza kuuliza hivi. Je serikali imeshindwa kumaliza tatizo la albino kwahiyo wanaeleza wazi kwa kulia?
Je huo ndiyo uwezo wa watawala wetu ulipofikia?

Wameshindwa,wamekwisha, tuwaondoe?
Unapomtaka mtu anayeuliza maswali kama NGURUMO akupe suluhisho ni lazima uelewe dhima ya MASWALI MAGUMU, ni lazima uelewa muundo wa kile kiulizwacho kuwa ndicho na kama sicho kisemwe kwanini hakijawa hivyo wakati mwonekano upo hivyo?

Hii inamaana kwamba kila jambo limeshindwa,tuanze upya?

Ngoja nimkumbushe huyo ajiitaye Prf UDSM, ubongo wa binadamu una akili na unaakisi mazingira yake, na ikiwa twadhani kuwa Prf UDSM ni kujua kutatua matatizo basi leo hii tusingelikuwa nayo.
Mfano simulizi za THE SMILE OF FORTUNE hadithi fupi iliyopo katika mkusanyiko wa hadithi fupi uliopewa jina la ENCOUNTERS OF AFRICA. simulizi zile hakuna tofauti na utawala wa awamu ya 4, ni yaleyale tuliyoaminishwa kwamba huyo ni mzuri kwetu bila kujihoji.

SASA, tukismea tusifikiri eti tutatue tu ilmradi kutatua maana yake nini?
Hakuna mantiki ya kuhoji na kutoa mwongozo wa kuuliza maswali?
Ni kweli kwamba serikali yetu imekosa tiba ya mauaji ya ndugu zetu hawa?
KWELI?KWELI?KWELI? kama kiongozi unalia kwa kushindwa kuonyesha njia, unawafunza nini wale waliotarajia uwaongoze?
ONDOKA WAPISHE WENGINE kwanini uongoze mahali ambapo panakushinda?
SITAKI kuamini eti tuhangaike wananchi milioni 35 halafu tuliowapa jukumu la kufanya mambo yetu waishie kulia kama wamefiwa na mababu zao?
Ikiwa tumeshindwa basi tuseme tumeshindwa.
Ajabu, mbona yule mwandishi Vick wa BBC alitusaidia mengi, lakini kwakuwa shibe ni siasa basi tumegeuka kuona hizo ni porojo huku ndugu zetu wanaumia.
Utaliaje kwa kuona kauli zako kama kiongozi zinatatanisha?
Je wewe ni mahakama hadi useme nao wauawe?
Basi hakuna maana ya sheria ikiwa mambo yenyewe ni hivi. Kila nikitafakari serikali hii, nasinyaa,nakonda,najiuliza kwanini zaidi ya milioni.
Samahani nimeshindwa kumaliza, nahisi kuhamanika na kudhalilisha nchi yetu kwa masuala madogo kama haya, labda tumsubiri Joji Kichaka aliyemaliza muda wake USA atusaidie, kulia.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'