Saturday, January 03, 2009

Wanataka tuote sugu?

Watawala wanapowatisha wananchi wasihoji, au wasifichue ufisadi, eti kwa kisingizio cha uchochezi, si bure kuna jambo wanaogopa. Na wakati mwingine wanataka wengine tuote sugu. Tukubaliane nao, tunyamaze?

4 comments:

MARKUS MPANGALA said...

Tuote sugu, tunyamaze tu tusiseme, yaani tuzoee shida. haa kwani shida zilikuwa kwajili yetu? kwanini tuote sugu huku wao wakijaribu kuondoa sugu zao. ToPIKI NZURI SANA HII. kazi njema

Anonymous said...

Hongera Ansbert kwa kazi nzuri na heri ya mwaka 2009! Jakaya ameishaona kuwa ana kazi kubwa mbele yake ya kudhihilisha kuwa yeye ni RAIS na hiyo kazi anaimudu; anataka kutumia vitisho mbele ya wanannchi ambao sasa wamegundua kuwa URAIS umemshinda na anachofanya sasa ni usanii tu. Hata hivyo bahati yake mbaya kwani watanzania ni wastaarabu na kama ulivyoseme mtu yeyete mstaarabu sio mwoga.Inaelekea kuwa mwaka 2009 utakuwa mgumu sana kwa Jakaya kwani vitisho vyake vitazua matatizo mengi sana ambayo yataleta madhara makubwa zaidi kwa utulivu wa nchi yetu zaidi ya mwaka jana.

Anonymous said...

nahisi unavuta bangi ww na kama huvuti basi ulishavuta mwandishi

Anonymous said...

We anonymous wa hapo juu, jadili hoja ya mwandishi, usionyeshe ujinga wako kwa kurusha matusi. Kama Ngurumo anavuta bangi kwa kuandika haya, nadhani aendelee tu, maana hata Nyerere alishasema kwamba wakati mwingine tunahitaji kuwa nan akili kama za mwendawazimu kuwakosoa CCM. Yeye wakati huo alikuwa anawakosoa kwa kutetea Azimio la Arusha walilolizika. Tanzania inahitaji kina Ngurumo kama 20 tu. Itabadilika. Elimu wanayoimwaga hapa haipootei bure labda kwa wasio na uwezo wa kuelewa kama huyo anonymmous hapo juu. Haishangaza Afrika inaendelea kudumaa....ndiyo sababu hata kina Mugabe wanaendelea kupata kura...ni za watu kama akina anonymous hawa...

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'