Sunday, February 04, 2007

CCM haina cha kusherehekea



Mwandishi mkongwe Yusuf Halimoja anatukumbusha kuwa Mwalimu Julius Nyerere (pichani juu), mwasisi wa CCM, alisema chama hicho kilianzishwa kujenga ujamaa, kulinda heshima ya Tanzania na kuwatetea wakulima na wafanyakazi. Baada ya miaka 30, je, kimefanikiwa? CCM ina cha kusherehekea? PATA JIBU.

1 comment:

Anonymous said...

Matembezi ya CCM Magu yadodoa

Na Anna Sunzula, Magu

WANANCHI na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachotawala Tanzania, hawakujitokeza kushiriki kwenye matembezi ya mshikamano ya kuadhimisha miaka 30 ya chama hicho wilayani Magu.

Kutojitokeza kwao kulimlazimisha Mkuu wa Wilaya hiyo, Mathew Nasei, kuhutubia mkutano ulikuwa na watu wazima wachache na watoto.

Matembezi hayo ya mshikamano yalifanyika Feb.04, kuanzia saa 12:00 alfajiri, yaligeuka kuwa kichekesho
pale wananchi na wengi wa wananchama wa CCM kutoshiriki, hivyo kulazimika kuwakusanya wachezaji wa timu ya mpira waliokuwa wameomba hifadhi ya kulala ndani ya ukumbi wa chama hicho siku hiyo.

Wachezaji hao ambao walikuwa wamevalia jezi za rangi nyekundu walijipanga katika maandamano hayo.

DC Nasei, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Magu na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Ngorongoro mkaoni Arusha, alifika kwenye uwanja na kuhutuba mkusanyiko huo mdogo ukiwa na idadi kubwa ya watoto.

Hali hiyo ilishangaza kwani hakukuwa na wananchi uwanjani na hata wale wachezaji mpira waliolazimisha kuandamana waliondoka baada ya kufika uwanjani na kwenda kuendelea na mazoezi yao.

Pamoja na uchache wa watu, katika hotuba yake, Nasei alisisitiza juu ya mshikamano na umoja miongoni mwa wananchi na CCM.

Baada ya kuhutubia, Mkuu wa Wilaya alitoa udhuru wa kutoendelea na ratiba iliyokuwa kutokana na kupata shughuli ya ghafla kikazi, kisha akaondoka.

Katibu Mwenezi wa CCM, Wilaya ya Magu, Dunia Mussa, alisema watu walishindwa kufika kutokana na wengi wao kuwa kanisani .

"Mimi nakwambia kuwa wananchi wote wako kanisani," alisema Dunia kwa mkato.

Wananchi waliohojiwa kuhusiana na kutofika kwao, walidai kwamba hakukuwa na hamasa yoyote iliyofanywa na uongozi wa CCM wilayani hapa.

Baadhi ya viongozi waliopo na nyazifa zao zikiwa kwenye mabano ni Dk Japhet ng'weshemi (Mwenyekiti wa
CCM wa Wilaya), Marco Kahuluda (Katibu wa CCM wa Wilaya), Lazaro Madata (Diwani wa Kata ya Magu Mjini
CCM) na Agnes Ezekiel (Katibu Tarafa wa Itumbili).hali hiyo, na kuongea na gazeti hili..

Imechapishwa katka gazeti la Mwananchi 7.2.2007

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'