Sunday, February 11, 2007

Ya Lowassa kama ya Sumaye?

Usishangae. Boksi hilo limejaa pesa taslimu. Lakini hiyo si hoja yangu hapa.
INASEMEKANA kuwa rada iliyonunuliwa na Tanzania kwa bei ghali, na ambayo inanuka rushwa, sasa ni mbovu. Ndege ya Rais, yenye utata na kunuka rushwa pia, haitumiki ipasavyo na inazidi kutafuna mabilioni ya wanyonge. Sasa limeibuka hili la magari ya kifahari ya Waziri Mkuu, Edward Lowassa. Kwanza ni ya bei mbaya; lakini si ya lazima. Zaidi ya hayo, wataalamu wanasema hayafai! Kwa mara nyingine, tumeliwa! SOMA HAPA. Hata Frederick Sumaye alianzwa hivi hivi.

2 comments:

Peter Nyanje said...

Mzee unatisha! Yaani huku hata wengine hawajaliona hilo gazeti lenye hii kigongo, we ushaidaka! Hongera.
Lakini hiyo ndiyo kasi mpya tuliyoahidiwa. Hata kabla wataalamu wa ulinzi hawajaulizwa kuhusu aina ya gari linalofaa, watu wanakuwa si tu wameshachukjua uamuzi, bali wamehsutakeleza. haina tofauti na muswada wa habari, kabla wadau hawajajua kinachotaka kufanyika, tayari muswada umeshachapishwa!

babo said...

huyu lowassa nae, mjanja sana anataka tu watu wampende, kula nchi tu ndo kazi yenu, na kufunika madhambi yenu.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'