Sunday, March 18, 2007

Inatekenya mbavu, au vipi?
MARA moja moja ni vema kujiburudisha kidogo, kucheka, kulegeza misuli na kupunguza tension. Katuni hii imetumwa kwangu na Peter Nyanje, ambaye ameipokea kutoka kwa wengine katika mzunguko wa kutumiana vichekesho. Nikaona vema niipatie mahali pa kutulia, ili wasomaji wa blogu hii, hasa wale ambao hawakupata na hawatapata 'bahati' ya kutumiwa katuni hii, nao wapate uhondo huu. BOFYA kwenye picha usome maelezo yake.

4 comments:

Michuzi said...

ansbert!

asisee nafurahi kusikia uko 'huru' ukibukua. kumbe ndo maana huonekani mjini. tupe vijimamboz vya huko basi

Bob said...

Hii hali! Kwa jinsi hii mafuta yote yatamkauka huyu jamaa, na itabidi abadilii surualii akirudi home - kwanza atakuwa ameifunga kwa kamba - maana hili lijamaa litakuwa limemtoa jasho.

Lazima hatakubali kukamatwa na hili lijamaa, hivyo lazima apungue. Hata likimkamata, hiyo shughuli atakayopewa si ya kawaida, Atakonda!

Mjengwa said...

Ansbert!
Vipi huko? Nafurahia kuingia humu kila nipatapo nafasi.

Suzary Justine said...

Hapo ndipo ilipo nguvu ya mwanamke. Au uwongo?

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'