Wednesday, March 07, 2007

TUENDAKO: Uchambuzi Bora kwa miaka 10

Nimesoma makala nyingi za Kibanda, kwa miaka 10 iliyopita. Ni mwandishi mzuri na makini. Lakini sijawahi kusoma makala yake nzuri kuliko hii hapa. Ameikuna akili yangu. Bofya hapa chini usome mwenyewe.

http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/3/7/makala7.php Soma pia nondo za Kibanda kwa JK katika mfululizo wa makala za TUENDAKO.

6 comments:

Anonymous said...

Hii chuma kweli. Ilishasemwa kwamba Ukweli utawapeni uhuru. Cudo Kibanda!

Anonymous said...

Makala safi sana,Chadema oyeee !!!!

Anonymous said...

Makala hii inafaa kutunzwa na kurejewa baadaye.

Anonymous said...

Kibanda anatisha jamani!!! Hizo data sio mchezo? au ana rafiki yake anafanya kazi usalama wa taifa? coz ni data za 'chini ya kapeti' kabisa!!

Anonymous said...

Kwani kujua masuala haya ndiko kuwa 'usalama wa taifa'? Kama mwandishi, anapaswa kuyajua haya. wala si yeye tu anayeyajua. Kwa taarifa yaho, waandishi wanawajua sana viongozi wetu. Tatizo ni kwamba hawaandiki hayo wanayoyajua, hadi wanapoamua, kama alivyofanya Kibanda. Angeweza kuacha na kufa nayo. Hii ndiyo sababu jamii huwa inawaheshimu waandishi, hasa wanapoamua kuwa wakweli na kulitumikia taifa kwa moyo mkunjufu usio na ushabiki wa chama tawala wala dola, kama wanavyofanya sasa na 'mzee wa tabasamu'.

Anonymous said...

hamu sana, shukrani

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'