Saturday, March 03, 2007

Zama mpya, majibu ya kizamani

Majibu ya kizamani, zama mpya! Inakubalika? Bofya hapa.

1 comment:

Anonymous said...

Umesema kweli Ngurumo. Hadi Watanzania tutakapoanza kufikiri wenyewe na kuepuka propaganda za wanasiasa, ndipo tutapata fursa ya kuendelea. Ilivyo sasa, nchi nzima imezamam katika ushabiki wa JK utadhani ametoka mbinguni. Mtu ambaye tumekuwa naye miak yote hiyo; hajawahi kufanya la maana, kwa wizara alizokabidhiwa aongoze, na hata kwa jimbo lake - leo anaonekana nyota, kila mtu yuko nyuma yake anapiga makofi! Leo amegeuka masiha, na wengine wamediriki kumlinganisha na Nyerere! Shxxxt!

Manyang'au nao hawaachi kumtumia. Wako nyuma yake, wengine ndio washauri wake wa karibu, wanatumia muda mwingi kumjenga JK kwa umma, ili wakati umma unazama katika ushabiki wa JK na CCM wao wanachukua chao mapema.

JK mwenyewe hana historia ya wizi - walau wa moja kwa moja. Lakini amzungukwa na wezi, na baadhi yao ndio walimpatia pesa za kampeni. Aseme atakacho lakini hawezi kuwatema, na watazidi kumchafua sasa au baada ya kuwa amemaliza muda wake.

Kasi mpya haipo, bali mbinu mpya za kunyakua huku wakishangiliwa. Nani hajuikwamba watu wale wale ndio wamemshauri JK atangaze kupitia mikatabaya madini, halafu hao hao wakasajili kampuni feki ya Richmond, naye akaikubali, ikapewa tenda, na sasa imeshindwa kazi? Ndani ya mwaka mmoja wa uongozi wake, kashfa kubwa kama hii inatafuta nini? Sisi tutabaki kuimbishwa 'kasi mpya' ambayo haipo.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'