Monday, March 12, 2007

Makala za kihistoria juu ya Chifu Marealle

Historia ni mama wa elimu yote. Zisome makala hizi mbili, utakiri hii ni sehemu nyeti ya historia yetu, katika nafsi ya Hayati Chifu Thomas Marealle. Anza na hii ya Kibanda, halafu malizia na hii hapa ya Halimoja.

5 comments:

Anonymous said...

Nina kila sababu ya kukubaliana zaidi na hoja ya Halimoja. Katika hali ya kawaida, Marealle anaonekana kujipigiai debe. Kama aliiwakilisha Tanganyika kule UN, alikuwa mwakilishi wa wakoloni. Nyerere ndiye aliwawakilisha Watanganyika kupitia TANU. Hivyo, si kweli kwamba Marealle alikuwa mpiganaji wa maslahi ya walalahoi. hana sababu ya kulalamikia kutohusishwa katika serikali ya Nyerere. Nyerere angeweza kumshirikisha, na angeweza pia kutomshirikisha, kama alivyofanya.

Anonymous said...

Ndiyo. Marealle alikuwa mjumbe wa Wakoloni hta alipokwenda Ghana,, ilikuwa vunga yao. Kama alikuwa mzalendo mbona hakukaa upande wa TANU. Kama tunampongeza Marealle kwa kwenda UNO, basi wapongezwe na wakoloni waliomtuma. Halmoja umefanya vizuri kuweka sawa historia iliyokuwa inapindishwa. Udumu!

Anonymous said...

Huyo Halimoja mnafiki anajifanya msemaji wa chadema,mtu akiketeta ccm msaliti ila yeye akisemea vizuri chadema sawa!watu wengine wanafikiri sijui wao wana akili sana,kwa kuwa wanajua kuandika?

Anonymous said...

Naamini mwandishi huyu hapa juu, anayeogopa kutaja jina lake, si mtetezi wa CCM. Naamini pia kwamba hata CCM hawawezi kumhitaji awatetee kwa sababu hana hoja, wala haonekani kama ana uwezo wa kujenga hoja. Anaonekana anaweza kurusha maneneo ya kitoto na ya 'kiswahili' tu, y akubeza kazi za watu, wakati yeye hafanyi kitu. Ukichunguza aina ya uandishi wake, anavyounda sentensi na kauli anazotoa, utagundua huyu ni miongoni mwa watanzania wengi mbumbumbu, wasiojua kinachoendelea, lakiniwapo tayari kulamba miguu ya wakubwa, ili warushiwe makombo. Ni mmojawapo wa watanzania wasioona mbali ya pua zao, wanaoishi ndani ya boksi, ambao kwa sababu hiyo, wanashangaa wanapokuatana na vijana wenye mawazo tofauti, wasiokubali kukumbatia jambo bila kuhoji, wanaopenda kutafakari na nkutafakarisha wengine katika jamii. Mtu huyu anajilinganisha na Ngurumo anajiona mnyonge, anaishia kurusha maneno ya kejeli dhidi ya Ngurumo na Halimoja, eti wanajifanya wanajua kwa sababu wanajua kuandika, eti wanafanya makosa kuikosoa CCM, eti wanaisghabikia CHADEMA. Huu ni wivu wa kitoto, ambao hata angewaua hao anaowachukia kwa kumzifi uwezo, yeye hawezi kuwa nan uwezo wao. Badala ya kuwachukia ni bora angejifunza kwao, akasoa vizuri maandishi yao na kupata la kujifunza na kuikomaza akili yake.

Hata Halimoja alipotaka kupingana na Kibanda, hakumtukana wala hajamjadili mwandishi, bali ameweka hoja zake kutokana na kumbukumbu za kihistoria alizonazo. Mwingine ambaye anadhani kwamba Halimoja amekosea, kama angekuwa ana AKILI na kuna anachojua ambacho kimekosewa, angeandika hapa na kumkosoa Halimoja kwa vielelezo, bila kumwita mnafiki. Kumwita mtu kama huyu mnafiki wakati wewe hujengi hoja, inaonyesha wewe ndiye mnafiki, kwa sababu unaonekana hakuna unalojua, na huna mchango kwa jamii, na bado unawakandia wanaokuzidi. Endelea kujiumbua hapa maana Ngurumo ametuwekea kijiwe hiki cha kukuza mawazo, utambuzi na fikra. wengine tunaingia humu kujifunza, maana yapo mengi tusiyoyajua. Hatuchangiiu kila hoja, hadi tunapochokozwa na wachangiaji wanaoandika bila kuwa na hoja, wanaotaka kutuharibika kijiwe chetu. Kama wametumwa, basi warudi wawaeleze waliowatuma kwamba kazi hiyo hawaiwezi kwa sababu hawana hoja za kujenga na kwamba hata kama wangekuwa nazo, uwezo huo Mungu hakuwajalia. Si wakubali tu kwamba hawajui?

Anonymous said...

Mawe hayo. Nayo hatarudia huyu mtoto, shabiki wa kasi ambayo haipo. AU akija atakuwa amekua ana hoja za kujenga badala ya maneno ya kitoto yenye kuakisi wivu alionao anaposoma kazi za wengine ambazo yeye hawezi kuzitengeneza.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'