Sunday, August 19, 2007

Habari Leo waua stori ya Zitto Kabwe


Magazeti ya serikali, Sunday News and Habari Leo Jumapili, 'yalikataa' kuandika habari za maandamano na mkutano wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, uliofanyika Dar es Salaam Agosti 18 kulaani hatua dhalimu ya Bunge dhidi ya mbunge huyo. AIBU!
Waandishi wao waliyashuhudia maandamano, mkutanoni walikuwepo, lakini walishindwa kutekeleza wajibu wao wa kitaaluma. UZALENDO uko wapi? Kama wanawadharau hao waliokusanyika kumsikiliza Kabwe, wanamwandikia nani?
Hata hivyo, mpiga picha wao aliweza kumshawishi mhariri wake kutumia walau picha inayoonyesha sehemu tu ya umati uliokusanyika Jangwani kumsikiliza Kabwe. Tazama mwenyewe.

6 comments:

Anonymous said...

Mheshimiwa Kabwe amedhihirisha kuwa wanamtandao maslahi wanatumia nafasi zao kulihujumu Taifa. Kwabahati mbaya Jakaya hana ubavu wa kuwadhibiti kwa kuwa hao hao ndio waliomfadhili mpaka akapata Urais!!! Kutegemea kwamba atawachukulia hatua yeyote ni kupoteza muda. Ni juu yetu wananchi kutambua kuwa CCM na serikali yake haipo kwa manufaa ya wananchi bali kwa hao wanamtandao tu.MUNGU INUSURU TANZANIA>

Anonymous said...

Kama Rais anafumbia macho ufisadi wa akinaKARAMAGI tafsiri yake ni nini? MAANA YAKE HAWA NI MAAGENT WAKE WA KUTUIBIA!!! Hivyo basi inawezekana Jakaya nae akawa kama Chiluba? Ndiyo kwasababu anawakingia kifua wezi.

Anonymous said...

Mimi kama Kijana wa Kitanzania ninayesoma na Kufatilia toka hapa Marekani chuo kikuu cha Colorado , sijafurahi hata kidogo na hali hii ya Uwezo wa bunge letu katika hili. siwezi kusema kuwa ndiyo democrasia hii hata kidogo. sisi tuliye nje ya Tanzania tunafatilia kwa makini sana habari toka huko tanzania na kuona kuwa mambo sio mazuri kabisa. tunashukuru sana gazeti la tanzania Daima kwa kuonyesha mtazamo mpya.
Josh Njogolo
Colorado

Anonymous said...

CCm wanajitapa, wanawadanganya wasioona mbali, lakini huu ni ushahidi kwamba mwisho wao wa kutawala nchi umefikia kikomo. Nguvu ya kuwaondoa tunayo, kwani si wao waliozaliwa kuwa watawala wetu. Tunahitaji mabadiliko, na wakati wenyewe ni sasa.

Anonymous said...

Nipo matembezini bado ila nafuatilia maswala kwa karibu. Sina mpango na CCM, kwa sababu za kueleweka, na sina mpango na Upinzani kwa vile na wao sera zao ni wazi wanachotaka ni kushika dola na wala si maendeleo yetu mimi na wewe Mtanzania.

Ila basi, ukweli haubadiliki kuwa yaliyotolewa na Mh. Kabwe na Slaa, yanahitaji kufanyiwa kazi jibu lieleweke. CCM badala ya kuyanfanyia kazi, wanaenda defensive! Mtu hauitaji mahesabu mengi kugundua mchezo uliopo hapa. CCM wanasambaratika kwa uwongo na hofu juu ya hofu.

Kazi ya kabwe na Idumu.

Anonymous said...

Tasisi, nadhani una hoja lakini inahitaji kukamilishwa. Mimi ninayeandika sina chama cha siasa, lakini naunga mkono jitihada za upinzani. Ndiyo njia iliyobaki ya kuwaondoa usingizini watawala waliolala.

Usiseme wapinzani hawana sera wazi. Zipo sana, lakini zitasaidia nini kama hawaingii madarakani. Au unadhani hayo maendeleo yako nayangu mimi watayawazia wapi na kuyatekelezea wapi kama sio madarakani?

Kwa jinsi mambo yanavyokwenda sasa, kazi ya kwanza iliyopo si kuimbembeleza wala kuionea aibu CCM, bali kuing'oa madarakani. Wakae wengine. Katka mchakato wa kuelekea madarakani sera zinaendelea kutengenezwa na kuboreshwa. Nia iwe kuiondoa kwanza CCM kwa sababu si wao pekee wenye uwezo wa kuongoza. Tanzania imejaa watu wengi wenye akili, waadilifu na wazalendo kuliko kundi hili la wana CCM walafi.

Kama wewe unadhani kazi ya upinzani ni kuwa na sera kwenye mafaili na kuziimba tu mikutanoni bila nia ya kushika madaraka, basi tutakuwa na upinzani maigizo. Kumbuka lengo la chama cha siasa ni kushika dola. Wananchi nao wakishaona chama hakina nia ya kushika dola bali kusindikiza, hawakiungi mkono.

Kama ni sera CCM wanazo vitabuni. Mbona zinawashinda kutekeleza? Hawana nia. Na zaidi ya hayo wamechoka, hivyolazima waondoke nchi ijipange upya.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'