Sunday, August 19, 2007

Karamagi anasafiri na mihuri yetu?


KAMA Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, anaweza kusaini mkataba wa madini nje ya nchi, London, Uingereza, wakati yuko ziarani na Rais Jakaya Kikwete, ina maana anasafiri na mihuri yetu? Pata uchambuzi wa swali hili HAPA, na toa maoni yako chini.

2 comments:

Anonymous said...

Karamagi alisafiri na mihuri miwili - mmoja ni huo aliotumia kusaini mikataba, na mwingine ni huo alioambatana nao ziarani - JK mwenyewe!

Anonymous said...

Kwa kweli zis iz veri denjarasi mwanawane,inakuwaje au ndio utaratibu wa wizara tusioufahamu watu wengi? hivi kusaini mkataba kama mhusika na mtia sahihi si kuna ulazima kidogo ukae ofisini tena kwako au kulikuwa na haraka sana ya kusaini huo mkataba.Na ni haraka ya wapi kwa sababu madini hayaozi si eti wajameni? kwa hiyo hata sisi kumbe huku kwenye maofisi tunaweza kutembea na mihuri tunagongesha tu issues juu kwa juu maana ndicho waziri anatufundisha hapa, hapa bwana inabidi watu sasa tuamke hamna swala la kukubali vitu viende tu sasa ndio nini basi hatuna haja ya kuwa na viongozi kila mtu aingie ikulu au wizarani ale kama wanavyofanya kwani nani anapenda kuwa maskini wa aidha kipato au kitu kingine, au hii nchi sasa inapelekwa na kila maamuzi ya kiongozi anavyotaka yeye? akilala akiamka wazo linalomjia ndio hilo hilo anatekeleza bile hata kujali maslahi ya nchi wala kushauriana na wananchi kaa mweee twaumizana namna hiyo!!!!!

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'