Thursday, August 30, 2007

Zitto apikiwa kashfa mpya


Habari zilizotapakaa ni kwamba wanamtandao, wakiongozwa na kinara wao, Rostam Azizi, wanapika kashfa mpya dhidi ya Zitto Kabwe (pichani kulia). Eti walitengeneza ya Amina Chifupa ikawalipukia na kuua mtu. Hawakuridhika. Wamejarbu kumdhalilisha Bungeni, akaibuka mshindi. Wananchi wanamshangilia, CCM wakazomewa. Sasa wamesikia Zitto na viongozi wa CHADEMA wanaanza kuzunguka mikoa 10 kuishitaki serikali kwa umma, wanamtandao wanakula njama mpya kwa kutumia baadhi ya vyombo vya habari 'kupika' kashfa mpya. Nia yao ni kupunguza imani ya wananchi na mvuto wa Zitto. Wamekiri, lakini inawauma, kwamba kwa sasa, Zitto amemfunika JK kwa mvuto.

Je, wahariri watakubaliana na mbinu za kina Rostam Azizi? Je, wananchi watamtosa Zitto? Kumkumbatia nani? Je, serikali itabadili sera zake kuhusu madini au itaendelea tu kuhangaika na namna ya kumsakama Zitto?

16 comments:

Anonymous said...

Rostam ndiye anayeichafua serikali ya JK. Katika hili la kuwaharibu wanahabari wetu, Rostam anaongoza kwa kutumia pesa kuua dhamira na taaluma zao, nao kwa kuwa wana njaa, na mioyo legelege, wanapokea na 'kumhudumia.' Ipo siku uchafu huu utawekwa hadharani, na mwisho wa ujinga wao utakuwa laana kwao. Siku hiyo yaja kwa kasi. Wasipoacha watajiju!

Anonymous said...

Hawamwezi Zitto kwa hili, wameshachemka, na wananchi wameshaamka. Pole yao!

Anonymous said...

Tatizo la vyombo vya habari vya Tanzania ni ushabiki wa kijinga kwa kushabikia hata yasiyoshabikika!! Rostam anashabikiwa na vyombo vya habari, lakini wanahabari hawa hawamjui vizuri mtu huyu!!! labda niwasaidie kidogo.

Rostam alizaliwa maeneo ya bukene nzega na wala si Igunga!! ukweli wa mambo ulivyo wazazi wake hawakuwa watanzania!! aliondoka nchim hii na wazazi wake kwenda kusikojulikana, kwa maana hii hata darasa la kwanza hajasoma hapa Tanzania!!! sina hakika hta huko alikokwenda na wazazi wake alisoma hata ile elimu ya msingi!!! kwa vile ukiongea naye lazima utagundua kwamba unaongea na mtu asiye na elimu kabisa, anajua tu kuandika na kusoma lakini hana elimu yoyote!!! hata hiyo masters anayoitaja kwenye tovuti ya bunge bila kutaja vyuo alivyosoma ni hadaa tu!!!hana elimu yoyote ya chuo kikuu!!!!

Alikuja nchini kwa mgongo wa ndugu zake, ili agombee ubunge wakati wa uchaguzi mdogo jimbo la Igunga kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wakati huo marehemu Charles Kabeho, ndugu zake walitaka wamwingize kwenye siasa ili alinde maslahi yao na pengine wanufaike kibiashara zaidi,ilionekana rahisi kwake kumwingiza kwenye siasa kwa vile hakuwa na chochote(mali)!!

Kwa kifupi mtu huyu kwanza uraia wake ni wa mashaka sana!!!kuna tetesi kwamba alivyoondoka nchini alikwenda Iran, hivyo ni raia wa Iran!!

Pili elimu yake haieleweki ni ya kiwango gani, ndio maana mara nyingi,hufanya lolote liwalo hasa kutumia fedha ili agombee peke yake kwa kuogopa mapungufu ya kielimu aliyonayo, pengine apite bila kupingwa wala kuulizwa sana kwa vile yuko peke yake!!!

Kwa ujumla hafai kabisa kuwa kiongozi kwa ngazi yoyote ile hapa nchini, inashangaza wanahabari wengine waliwahikuandika eti alitarajiwa kuwa waziri wa fedha!!! kama ccm wangefanya hivyo bora mtu kuhama nchi hii,kuliko kuongozwa na watu wa aina hii!!

Haya ni machache sana, wanahabari mchunguzeni vizuri rostam mtajua mengi juu yake!!

Anonymous said...

Jakaya amekiri hadharani kuwa Rostam ni rafiki yake mpenzi kwa hiyo yote anayofanya yana blessings za Rais wetu na ndiyo maana akamteua kuwa Treasurer wa ccm akifanya kazi karibu sana na Treasurer wa serikali ambaye ni waziri wa Fedha. Huyu Rostam anajulikana kama mfanya biashara lakini kwa biashara anazofanya hawezi kwenda nchi za ulaya magharibi watamkamata!!! Sasa huyu ndiye mshauri wa Rais wetu !!! Tumeliwa.

Anonymous said...

Jakaya amekiri hadharani kuwa Rostam ni rafiki yake mpenzi kwa hiyo yote anayofanya yana blessings za Rais wetu na ndiyo maana akamteua kuwa Treasurer wa ccm akifanya kazi karibu sana na Treasurer wa serikali ambaye ni waziri wa Fedha. Huyu Rostam anajulikana kama mfanya biashara lakini kwa biashara anazofanya hawezi kwenda nchi za ulaya magharibi watamkamata!!! Sasa huyu ndiye mshauri wa Rais wetu !!! Tumeliwa.

Anonymous said...

Hii habari ya Rostam kutumia hela kuharibu nyanja ya habari, kutaka kufanya magazeti yoye kuwa ni kama Uhuru nilikuwa siijui undani wake. Lakini sasa mambo yanaanza kuwa wazi. Madaktari wa ku-spin wameingia nchini...kweli ni kasi mpya.

Bob Sankofa said...

Unaposhindwa kusoma nyakati hata uwe umefika Chuo Kikuu unakuwa ni mbumbu tu.

CCM pamoja na kuwa chama tawala toka uhuru wa nchi hii, tangu Mwalimu anaa'tuke madarakani imeshindwa kusoma nyakati.

Zitto anazisoma nyakati, anajua wapi aguse ili kuimegua CCM. CCM wameshindwa kujua katika kila ZITTO mmoja kuna kina ZITTO kumi nyuma yake.

Vyombi vingi vya habari bado viko fungate na serikali, navyo vinashindwa kusoma nyakati. Matokeo yake magazeti ya udaku vinawapiga bao la kisigino.

Ongea na mama lishe au wamachinga amabo ndio sehemu kubwa ya watu waliompatia "White" asilimia zadi ya 80 ya kura za urais wake ndio hapo utajua kuwa CCM inasoma nyakati au inaishi juu ya umaarufu wa waliotutangulia badala ya kuuendeleza.

Zitto atawagaragaza hadi macho yawachomoke

Anonymous said...

Sikubaliani na yale aliyoandika kalundi hapo juu, Kikwete hajawahi tamka kwamba Rostam ni rafikiye mpenzi, ni rafiki kama rafiki wengine tu, wala kuwa rafiki yake Kikwete hakumpi vote ya kufanya lolote analotaka, si kweli.

Sikubaliani pia kuwa treasurer wa ccm anafanya kazi kwa karibu na waziri wa fedha, uhazini wa chama ni wa chama tu, muundo,sera na utendaji vinatofautiana sana!!!lakini pia maneno aliyotumia kwamba "sasa huyu ndiye mshauri wa rais - tumeliwa" ni ya kutaka kuwafanya watu wakate tamaa(character assassination)

Rais kikwete alitamka bayana kuwa hana ubia na mtu yeyote kwa cheo alicho nacho!!!

Ina maana Rostam is nobody!kwenye masuala yanayohusu maslahi ya taifa!!!hata na rafiki zake wengine!!

Tatizo lililopo kwa mtazamo wangu ni udhaifu kwenye state machineries hasa idara ya usalama wa taifa!!ambayo ina jukumu la kuhakikisha usafi wa serikali kwenye maeneo yote!!!ni wajibu wao kuhakikisha kwamba rais anazungukwa na watu safi wasio na dosari yoyote!!!

Kwa kifupi maslahi ya taifa ni muhimu zaidi kuliko marafiki wa rais!!!

Anonymous said...

I stand by my Statement bwana Prosper that Jakaya minced no words in stating that Rostam and Edward Ngoyai were his bosom friends and this he did when he was asked by jounals about his relationship with these two guys wakati wa mchakato. Kutamka na kutenda are two different things. Rostam na Karamagi are bisiness partners huko kwenye CONTAINER TERMINAL na JAkaya ni mbia huko Buzwagi nini, mbona badala ya kuwa mkali kwa hawa wezi siku hizi anakuwa mkali kwa wananchi wanaomunesha mabango ya kero zao??? wanapomuonesha mabango!! Hii yote inaonesha frustrations alizonazo kutokana na wasaidizi mafisadi; Lakini kwasababu aliingia na baggage ya watu waliomfadhili kupata urais nao sasa wanataka kurudisha hela yao na Kinara wa kufanya yote hayo ni kijana wa kiburushi aitwae Rostam.Kuwa Roatam anafanya kazi karibu na Zakia wala hiyo sio siri, Kila jumatatu asubuhi yuko Hazina!!!

Anonymous said...

I stand by my Statement bwana Prosper that Jakaya minced no words in stating that Rostam and Edward Ngoyai were his bosom friends and this he did when he was asked by jounals about his relationship with these two guys wakati wa mchakato. Kutamka na kutenda are two different things. Rostam na Karamagi are bisiness partners huko kwenye CONTAINER TERMINAL na JAkaya ni mbia huko Buzwagi nini, mbona badala ya kuwa mkali kwa hawa wezi siku hizi anakuwa mkali kwa wananchi wanaomunesha mabango ya kero zao??? wanapomuonesha mabango!! Hii yote inaonesha frustrations alizonazo kutokana na wasaidizi mafisadi; Lakini kwasababu aliingia na baggage ya watu waliomfadhili kupata urais nao sasa wanataka kurudisha hela yao na Kinara wa kufanya yote hayo ni kijana wa kiburushi aitwae Rostam.Kuwa Roatam anafanya kazi karibu na Zakia wala hiyo sio siri, Kila jumatatu asubuhi yuko Hazina!!!

Anonymous said...

Kalundi, nadhani uko sahihi. Mbona imesemwa sana hata kabla ya kampeni kuanza kwamba Rostam "anamlamba" mama mafweza (hapo alikuwa hajawa maa mafweza)? Wengine waliguna wakidai Rostam ni mdogo kwa bibie, lakini pesa si unajua tena? Halafu huyo mama si ndiye alikabishiwa mikoba ya Bi Salma ili amfunde namna ya kusimama jukwaani kutafuta kura za mumewe huko Kusini?

Zipo kauli pia zinazosambaa kila siku kwamba waziri halisi wa fedha ni Rostam kwa sababu ya uhusiano wake na mama fweza, na kwa sababu ya ukilaza wa mama fweza katika masuala ya fedha na uchumi.

Sasa Kama Jakaya alisema hana ubia na mtu maana yake hana? Mbona sisi tunaona ubia upo na ndio unamfanya ashindwe kuchukua maamuzi ya maana? Mbona tunawajua waliomchangia fedha za kampeni hadi akaacha kutumia za CCM zilizokuwapo? Na Waarabu wamo, na aliyetumia ni Rostam, sasa huyu jamaa anataka kutetea kauli au vitendo vya Jakaya? Watanzania wa leo hatudanganywi kama wa zamani bwana...kumekucha!

Anonymous said...

Nadhani bwana Kalundi yuko sahihi sawia ,na kweli kama asemavyo Prosper kuwa usalama wa Taifa unatakiwa kumlinda Rais dhidi ya mafisadi; lakini je usalama wa Taifa watafanyaje kazi hiyo kama hao mafisadi ni mawaziri na Treasurer wa CCM? Kazi ya usalama wa Taifa inakuwa ngumu kidogo kuwazuia hawa jamaa kuingia IKULU. Ndio maana Mheshimiwa huyu anasema TUMELIWA!! Hii sio character assasination kama anavyodhani Prosper bali ni statement of fact.

Anonymous said...

Siriha, unajua, bwana prosper anadhani hatujaamka. Tumeshajua ujanjaujanja wao, kutoa kauli tamu huku nyuma yake umefichika ukora wa ajabu. Zaidi ya hayo, hawa watu wenyewe tunawaelewa vizuri, na nia yao tunaijua maana wameanza kujifunua pole pole, licha ya nguvu yao kumeza vyombo vya habari. Wanateteana tu kwa sababu wanajuana kwa vilemba vyao!

Anonymous said...

Napenda sana kuona kuwa watu kama wakina zitto kabwe, wanasimama Imara sana huko Tanzania. Hivyo kuna Haja ya watu kubadilika kama tunataka kweli maendeleo ya kweli.. Hivyo umefika wakati sisi kama Watanzania kuona kuwa viongozi wetu ni wasaliti kwetu.
Josh Michael
marekani

Anonymous said...

nyie acheni kabisa kusapoti wahuni hawa wao wanakashifu wakishakosa kazi na kuhusu rostam azizi ni mtu ambae serious hana shida yapesa ya umma nyie hamumjui hebu nyamazeni mmnarookwa tu mimi namfahamu na najua jinsi gani anasaidia watu mbali mbali

Anonymous said...

Bwana anonymous uliyetangulia, pole sana. Hii inaonyesha kwamba humjui Rostam, na kile unachokijua ndicho hicho kidogo kinachokudanganya, just a tip of an iceberg. Unasema Mr. Richmond hana shida napesa ya umma? Anatafuta nini kwenye Dowans na kwenye madini yetu? Hujui hata amefikaje hapo alipo...Kaa kimya labda kama na wewe ni mwizi mwenzie au unafaidi makombo ya wizi wake. Kumbuka hata wezi na majambazi husaidia watu na hutoa sadaka kubwa.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'