Friday, September 10, 2010

Dk. Slaa akemea majini ya Sheikh Yahya Hussein


Dk. Willibrod Slaa amemkemea mnajimu Sheikh Yahya Hussein (pichani) aliyeahidi kumpa Rais Jakaya Kikwete 'ulinzi wa majini,' ili kukabiliana na nguvu za giza zinazomwandama na kumwangusha majukwaani. Akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Katoro, jimbo la Busanda, Mwanza, Dk. Slaa alisema "nchi haiwezi kuongozwa na uchawi. Haiongozwi na imani za watu, kila mtu ana imani yake, lakini tusifike mahali tukaongoza nchi kwa uchawi."

Alimtaka Rais Jakaya Kikwete kumkemea Sheikh Yahya kwa kauli hiyo iliyotolewa juzi Dar es Salaam, la sivyo wananchi wataamini mnajimu huyo anatumiwa na CCM kuleta hofu katika jamii. Aliwakumbusha wananchi kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, Sheikh Yahya alisema mtu yeyote atakayegombea urais na Kikwete, atakufa. Dk. Slaa alisema: "Sisi wengine ni majabali, hatuogopi."

3 comments:

NN Mhango said...

Nani amkemee nani iwapo wote lao moja? Yale ya maruhani ya Zenj sasa yametua bara. Kikwete, kutokana na kuvurunda alikoonyesha, hana ubavu wa kumkemea Yahya Hussein kwa kuogopa asitoboe mengi ayajuayo kuhusiana na mteja wake huyu. Inasikitisha hata daktari wa Kikwete ameshindwa kukemea maana ameingiliwa kazini. Hii ndiyo Danganyika inayopaswa kukombolewa na Daktari Wilibrod Slaa. Na wananchi wajue. Fursa kama hizi hujitokeza mara moja kwa muhula.

stans said...

who da hell is this yahya...he wants pipo 2 bliv in uchawi au nin????nafikiri anasema hvyo kwa kuwa anajua katumwa na nani aseme hvyo ni mwenzao huyo analipa fadhila za kulipiwa dola 10000 kwenda kujitibia india

Anonymous said...

ENEEEEEZEEENI!

MIRAJI KIKWETE na wenzake wako kama 10 wanacheza na daftari la wapinga kura,mtashangaa wenyewe maana pia wanacheza na server ya NEC wameongeza namba ya wapiga kura kutoka mil 16.5 mpaka mil 19. kama mna uwezo ofisi yao iko ukipita jkt mlalakuwa turn left nr keys hotel

Napenda kuwajulisha mikakati michafu ya kupora na kuzuia maamuzi ya umma yanayofanywa na ccm kwa uratibu wa usalama wa taifa. Baada ya kubaini dalili za kuanguka vibaya katika uchaguzi wa mwaka huu idara ya usalama wa taifa imeandaa mikakati ya kuiba kura ili kuzuia chadema msiingie ikulu. Mikakati hii inaeleweka vizuri kwa tume ya taifa ya uchaguzi ambayo inashirikiana bega kwa bega na idara ya usalama wa taifa kumtengenezea jk ushindi bandia wa 80%. Wana hakika watanzania watagundua wizi huo na watakataa matokeo ndiyo maana kwanza waliwatumia viongozi wa dini waliotembelea makao makuu ya chadema wawasihi chadema wakubali matokeo yatakapotangazwa na juzi wamelitumia jeshi kutisha wananchi watakaoamua kupinga matokeo ya kupikwa yanayoandaliwa na nec/usalama wa taifa.
Majid kikula ambaye ni government security officer ndiye mratibu wa zoezi la kuiba kura, ni mtaalamu aliyebobea katika kazi za aina hii aliratibu vizuri zoezi kama hilo mwaka 2005. Pia mwaka 2007 alitumwa kenya kwenda kumsaidia kibaki kupora ushindi wa odinga.Kikula anatumia muda wake mwingi hivi sasa ofisi za tume ya uchaguzi kwa ajili ya uratibu wa uvurugaji daftari la kudumu la wapiga kura akiifanya kazi hiyo kwa karibu na baadhi ya watendaji wa nec na maafisa kadhaa wa usalama wa taifa kutoka kurugenzi ya IT ya idara ya usalama (DITA) ambao wako ndani ya nec kwa zaidi ya miezi sita sasa,nitawapatia majina yao .
Pia kuna vijana wataalamu wa IT waliochukuliwa kutoka maeneo mbalimbali wamepewa nyumba upanga mtaa wa undali shughuli kubwa wanayofanya ni kuandaa utaratibu wa ku-access remotely daftari la kudumu la wapiga kura. Hawa wanafanya kazi chini ya salva rweyemamu na mindi kasiga kutoka kurugenzi ya mawasiliano ikulu.Wapo vijana kadhaa leo nawapa majina ya wawili; maharage chande na edgar masatu wanafanya kazi kwa karibu na nzowa wa idara ya usalama ambaye ndiye aliyeratibu shambulio la kumwagiwa tindikali kubenea. Pia kuna kundi linalojumuisha wataalamu wa printing wa kiwanda cha uchapaji cha usalama wa taifa kilichopo MALINDI ambao hivi karibuni walikuwa mjini tanga kwa semina fupi ya jinsi ya kughushi kura kupitia fake ballot paper, timu hii inaongozwa na ndg SINYAU.
Kwa hiyo utaona kwamba imeandaliwa mikakati mingi kuufanikisha uovu huo ili mmoja ukikwama basi mwingine utatumika ila wameamua ni lazima jk ashinde kwa 80%. Ndani ya idara ya usalama wa taifa maafisa wengi wamechoshwa na uongozi mbovu wa ccm hivyo wanataka mabadiliko ya uongozi idara imechukua hatua kadhaa kuhakikisha maafisa wote wa idara wanampigia kura jk, wote wameagizwa kuwasilisha vitambulisho vyao vya kupigia kura ili vinakiliwe namba ili atakayepigia upinzani afukuzwe kazi baada ya uchaguzi.
Fuatilieni kwa karibu haya niliyowaeleza nimeyapata kwa nafasi yangu ndani ya tiss. Huyu KIKULA mfuatilieni kwa karibu ni hatari. HAKIKISHENI DUNIA NA WATANZANIA WOTE WANAJUA MAPEMA HILA HIZI. Jambo la kujiuliza maafisa usalama wa taifa wanafanya nini ndani ya tume ya uchaguzi wakati huu.

Jamani watu wa MUNGU ebu tuvunjeni hali hii maana tukiinyamazia itakuja kutugharimu mbeleni.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'