Sunday, September 12, 2010

Hii ndiyo Bunda ya Dk. SlaaLeo tuko Bunda. Acha picha hizi ziseme zenyewe. Maelezo mengine baadaye. Itoshe tu kusema kwamba miongoni mwa maelfu ya wana Bunda waliofurika kumsikiliza Dk. Slaa katika viwanja vya Sabasaba ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Francis Isack. Alikaa jukwaa moja na Dk. Slaa, naye alimsifu kwa ukomavu wa kisiasa, lakini akamuonya kwamba kama alikuwa amekwenda pale kwa nia tofauti, atazame umma, apime nguvu yake na apeleke taarifa za kile anachosikia na kuona. Alimsimamisha DC huyo akawasalimia wananchi kwa kunyosha mikono juu.

2 comments:

Anonymous said...

Unguruma Baba, Unguruma wewe ni Dume kweli kweli, Rais ni Dr. Slaa nawasihi wenzangu hamtajuta kumchagua mtu makini na wabunge wake makini madiwani makini kutoka CHADEMA tu na si mahala pengine sasa jichanganye kwa hizo kapelo na buku tano tuone miaka mitano utavuka na hiyo buku tano yako?
kwa Mh. Dr. Slaa ni maisha ya uhakika hakuna utapeli hapa, kumbuka hata UDr. wake si wa zawadi kama wengine wanaopewa kwa sababu ya uongozi ambao ni sifuri. JK jamani ni mtalii!! Hana dili yoyote tena ni mtu asiye na maamuzi ndiyo maana hata mawaziri wake wanapiga dili chafu atawafanya nini?
KURA YAKO NI KWA CHADEMA PLEASE.

Anonymous said...

31 Octoba 2010, masanduku ya kura yatapasuka. Tunajua wanaiba sana kura, lakini watapata salaam. Wasimamizi wetu muwe makini. NEC msijiume kuutangaza ukweli. Tumechoshwa na SANAA + UTALII! Tunataka kazi tena zenye tija kwa wananchi, tutadhihirisha hilo Octoba 31.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'