Monday, September 06, 2010

JK hawezi kushinda bila njama chafu?

SIJUI kwa nini JK na wapambe wake hawajifunzi. Mwaka 2005 walilazimika kumwita Dk Salim Ahmed Salim "mwarabu na muuaji wa Rais Karume." Naamini laana ya Dk. Salim imekuwa inamwandama JK kwa miaka yote minne. Na sasa baada ya kuona upepo mkali dhidi ya JK, na kama vile hawana uwezo wa kujifunza, wameanza kumshambulia binafsi, Dk Slaa. Lakini kwa bahati mbaya, aina hii ya mashambulizi itakapogeuzwa na kuelekezwa kwa JK, watakuwa wamemmaliza mtu wao. Najiuliza: Hivi JK amechoka kiasi hicho?

2 comments:

Stella said...

Si Jakaya Kikwete tu aliyechoka, bali CCM yenyewe kwa kumchagua kuwa mgombea wao wakati wakijua fika kuwa uongozi wake wa miaka mitano Ikulu ulikuwa mbovu.

CCM walipaswa kusoma alama za nyakati na kufikiria kumpumzisha JK.

Cha kushangaza ni chombo cha habari cha umma - TBC1 - kuonyesha udhaifu wa 'coverage' kwa kutangaza habari ya hitilafu ya helikopta ya CHADEMA kwenye taarifa ya habari (Jumapili tarehe 05.09.2010, saa 2 usiku) badala ya kutangaza sera za mgombea Urais wa CHADEMA. Kwa TBC1 habari muhimu kwa wananchi ni helikopta na si sera za chama ambazo wananchi watazitumia kuamua nani wamchague kuwa kiongozi wao.

makanika said...

Tumewachoka hawa wakaramba wa CCM
chagua Kikwete chagua Kikwete, naomba kura zenu, kama umefanya mazuri huna haja ya kutukana wengine na kubembeleza kura kwa watoto wako si wanakujua manjonjo uliyowapa nao bila ya kuwaomba ni wajibu wao kukupa kura ili umalizie mambo uliyoanza kuwafanyia, yanini unahangaika kuomba kura? mfanyakazi anastahili posho yake.
Gregory Haule, dsm
0655102101

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'