Saturday, September 04, 2010

Tendwa aalikwa Ikulu kuteta na JK

MSAJILI wa Vyama Vya Siasa, John Tendwa, ameonekana Ikulu. Alikwenda kukutana na Rais Jakaya Kikwete Alhamisi majira ya saa 9.00 alasiri. Wachunguzi wa mambo wanasema wito wa Tendwa Ikulu una uhusiano na pingamizi la Chadema dhidi ya JK, ambalo limeikalia vibaya CCM, na linatarajiwa kutolewa jibu na Tendwa Jumatatu keshokutwa. Kama haki itatendeka au la, ni jambo jingine; na matokeo yake yatajulikana hapo baadaye. Je, yawezekana Tendwa anajipalia mkaa? Kama hakutarajia, sasa hana ujanja. Tumeshajua!

12 comments:

mkibunga said...

mbona hilo liko wazi kuwa tendwa atasema hivi:madai ya chadema hayana msingi rais hajatenda kosa ILA Tendwa jua kuwa hata ukifa kaburi lako litafukuliwa na kuadhibiwa wewe,makamba,kingunge,chenge,LOWASA, rostam,tambwe,YA kikwete ni sawa na ya kibaki alipolazimisha aapishwe na wewe umemwita tendwa kumpa majibu lakini kila jambo lina mwisho yuko wapi mkapa,kamandoo,macela

Anonymous said...

ngurumo, ni mzuri wa kupamba. lkn ni mvivu wa kufikiri
sijui huoni udahaifu wa dk slaa ndio kila maana unamsifu, kumsifu kwenda mbele

www.jktu2010.blogspot.com
malariasugu@jamiiforums.com

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

wakati ukuta....utaamua yote!

EVARIST said...

Asante sana kwa kutuhabarisha.

Anonymous said...

Du mapaparazi wameshammulika. Haya ngoja tusubiri tuone maamuzi yatakuwaje, Ila ndio hivyo kesi ya Mbuzi kupelekwa kwa Chui unategemea nini, anyway tusiandikie mate.........

Mdau UK BK

Stella said...

Malariasugu, una haki ya kusema kuhusu Ngurumo. Umeanzia kwenye JAMIIFORUM hadi huku kwenye blogu yake. Sawa, unayo haki; lakini je ni kweli unayosema? Kwamba Ngurumo ni mvivu wa kufikiri? Kwa vile umeweza kufika hadi kwenye blogu, basi wewe mwenyewe acha uvivu ufuatilie maandiko yake mengi humu humu - kwa ushauri anzia mwaka 2005.
Kuhusu kumpamba Slaa, ni haki ya Ngurumo kama ilivyo haki yako na mimi kumpamba mtu anayestahili kupambwa. Sasa unataka ampambe JK kwa lipi? Au kwa kuudidimiza uchumi na kutalii nje ya nchi wakati maisha ya Watanzania yanazidi kuwa magumu? Hujui wananchi wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku? Au ampambe kwa kutoa rushwa kwa wafanyakazi kwa kuwaongezea mishahara wakati huu wa kampeni kana kwamba si haki yao ya msingi?

Basi leo tumemsikia huyo Tendwa akitekeleza hayo aliyoagwizwa na yule bosi wake kwenye kifafa

Stella said...

Blogger, I beg your pardon - is it possible not to publish comments more than once? Is it the publisher's fault? Excuse me!

Stella said...

Tendwa amewatenda wapenda demokrasia ya kweli!

Majibu ya msajili wa vyama vya siasa yalitegemewa kwa vile sote tunajua kuwa asingemsaliti mwajiri wake naye akasalimika.

Tendwa amedhihirisha wazi kuwa yeye bado ni mwanaCCM. Hivi kweli JK kutangaza mishahara mipya pamoja na ahadi nyinginezo wakati akiomba kura kwa wananchi hajakiuka sheria ya uchaguzi 2010?

Haki ya kuongeza mishahara na kwa kiasi alichotaja ameipata wapi? Kwenye kikao kipi na cha bunge lipi? Nyongesa ya mshahara ni haki ya wafanyakazi, lakini si kwa njia ya rushwa. Ni haki yao stahiki.

Time will tell, mazuri hayaji ghafla, huchukua muda ili yawe mazuri kweli kweli.

Anonymous said...

tendwa ni kibaraka wa CCM hilo lipo wazi nakumbuka baada JK kutangazwa mshindi katika uchaguzi mwaka 2005 nilimuona live akishangilia ushindi huu, leo hii aweze kutoa haki huyu!! na kuna baadhi ya waandishi rushwa wanapenda kutetea hata vitu vya kijanga, nawashauri kuwa DHAMBI HIZI WATARIDHISHA NDUGU ZAO PAMOJA NA FAMILA ZAO WAKATI WAKIWA WAMEMALIZA MAISHA YAO. PEOPLES POWER, Sauti ya Watu WATIIFU NA WEMA NI Sauti ya MUNGU.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'