Ndesanjo ametema cheche katika gazeti la Mwananchi Jumapili Februari 18, 2007. Makala yake niliiunganisha hapa, lakini baada ya Jumapili kupita, ikawa haipatikani tena. Sasa ukibofya, inakuja nyingine mpya; nikaamua kuhariri na kuiondoa. Nadhani wataalamu wa tovuti ya Mwananchi wanapaswa kujua kuwa tovuti yao haitunzi kumbukumbu za nyuma; warekebishe kasoro hiyo. Lakini hoja ya Ndesanjo ni kwamba Watanzania wasiwe wanachukia tu maovu ya watawala wao, wanalalamika, halafu uchaguzi ukifika wanawarejesha madarakani. Wawaondoe. Anasema ni vema waanzie kwenye serikali za mitaa, si Ikulu tu. Makala inasisitiza kile ambacho mwandishi mwingine, Ndimara Tegambwage, hupenda kukiita 'kuchukia na kuchukua hatua.' Kama unaweza itafute uisome mwenyewe. Ni tamu!
1 comment:
Mdio Ngurumo. Kuchukia kuwe ndio mwanzo wa kuchukua hatua. Chukia, chukua hatua. Nimeupenda msemo huu.
Post a Comment