Sunday, March 04, 2007

Tukubaliane, hatuna Wimbo wa Taifa

Unajua kwamba Watanzania hatuna Wimbo wa Taifa? Bofya hapa uone sababu.

11 comments:

Anonymous said...

Siku Chama chako chadema kitakapo tawala watabadilisha,wakati huo wewe utakuwa waziri wa habari na utamaduni chini ya utawala wa "Rais"Mbowe

Jeff Msangi said...

Ngurumo,
Una mantiki katika unachokiongelea katika makala yako.Hata hivyo sioni ubaya wa kuendelea kuutumia wimbo wa taifa kama ulivyo hivi leo hata kama tumeiga tune kutoka Afrika Kusini.Kwanza wimbo unasema Mungu ibariki Afrika na sio ibariki Afrika Kusini au ANC.Afrika ni yetu sote kwa hiyo kama ni kosa alifanya mtungaji wa wimbo.Kwa kutumia neno Afrika aliishirikisha Afrika nzima.Lakini pia sio vibaya kama tukisisitiza kwamba kila baada ya Mungu ibariki Afrika lazima Tanzania,Tanzania ifuatie(kama ilivyo hivi sasa nadhani)

Anonymous said...

Hakuna wimbo naupenda kwa wimbo wa taifa wa Tanzania,labda ukubaliane wewe na mbowe kama hatuna wimbo wa Taifa, mtakapowala chadema badilisheni wimbo wa taifa,siku na kuwa mwenyekiti wa chadema nabadilisha ile bendera ile siyo bendera hakuna bendera naye ichukia kama ya chadema ,wana chadema wakubaliane hawana bendera

Anonymous said...

Bwana Ngurumo, mimi ni msomaji wa mara kwa mara wa blogu yako, ingawa huwa sichangii sana. Naridhika na uchambuzi wako, katika mada unazotoa, zinazofikirisha kwelikweli. Leo nimeamua niandike, si kuchangia mada, bali kwa kuwa kuna msomaji mmoja mpuuzi nimemkuta hapa. Nimesoma mchango wake hapo juu, amechangia mara kadhaa akisema kitu kile kile. Wakati ni sahihi kutambua kuwa akili ni nywele, na kila mtu ana zake, mwenzetu huyu ameonyesha udhaifu mkubwa. 1. Anadhani wimbo wa taifa uliopo ni wa CCM. 2. Anadhani critique uliyoitoa ni ya ki-CHADEMA; anamwoma Mbowe katika uchambuzi wako. 3. Anafikiri kwamba kila anayetoa changamoto ni mbaya wa CCM.

Lakini pia kwa jinsi anavyoandika, anaonekana kama mtu mwenye upeo mdogo, na anajitambulisha kama kada wa CCM. Nimerudia kusoma uchambuzi wako, sikuona kama ulikuwa unaijadili CCM. Ameshindwa kucheua ulichoandika, kakimbilia kwenye ushabiki wa vyama. Ndio watanzania wenzetu hao - si ajabu naye yu miongoni mwa 'wasomi' wetu!Hayuko peke yake. Bila shaka tutawaona na wengine.

Anonymous said...

Hivi watu wengine wakoje? Sasa hapa kuna uhusiano gani kati ya article ya Ngurumo na Mbowe na Chadema? Kumbe nchi yetu imejaa wapuuz, na bahati mbaya baadhi yao ndiyo wanaotuongoza! Mtu kajenga hoja. Wewe huna hoja, si unyamaze tu ujilaumu kwa kutoelewa mambo?

Nimekuwa msomaji mzuri wa article za Ngurumo tangu akiwa RAI. Ni mawe mazito, tofauti na makala nyingi za kujikomba tunazoziona kwa waandishi wengi nchini. Nchi yetu inahitaji vicha vya namna hii. Hongera Ngurumo!

Anonymous said...

Kabisa umenena

Anonymous said...

Anayepinga hili ni mmojawao, hao wanaosikia lakini hawaelewi; wanaotazama lakini hawaoni. Achana naye; amechelewa. bado yu gizani. Haulingani akili, wengine huwahi na wengine huchelewa kuelewa hata jambo dogo kama hili. Ngurumo endelea kutwanga kazi...

Anonymous said...

mpuuzi huyo...tuawajua haa ndio zao...kulamba miguu ya wakubwa, hata michafu! Wazo la kjitegemea kimawazo na kimsimamo lilikufa zamani katika akili za baadhi ya watanzania, hasa wanaotarajia kurushiwa makombo na walo madarakani. Ngurumo, chapa kazi, wenye akili wanasikia na wanafuatilia hatma ya nchi. The country is going to the dogs!

Anonymous said...

Sikuwahi kulifikiria suala la wimbo huu kwa mtazamo huu. Hivi wimbo wa Tanzania nakupenda ulitungwa na nani? Isije ukawa huu nao ni wa kuazima.

Anonymous said...

hivi wanajikomba kwa mbowe hawapo?
Mbona mbowe hakosolewi na ngurumo?au mbowe malaika?msfikri watu matahira?Ngurumo tunataka makala ya kukosoa chademaaaa
CCM waovu sawa,kikwete hafai sawa!Sasa tunataka makala ya kuikosoa chadema na bwana wenu mbowe!yuone kama una ubavu huo.

Anonymous said...

Acha ushamba wewe! Ngurumo amkosoe Mbowe? Kwani Mbowe ni nani? Mwenye ridhaa ya Watanzania ni Kikwete. ndiye mwenye dhamana, anayeshikilia 'roho' za Watanzania wote, ukiwamoo wewe. Huyu ndiye mashi tuliyeahidiwa, ambaye mwaka umepita sasa anachekacheka tu! Asiandamwe yeye aandamwe Mbowe, mwanafunzi wa shule?

Au wewe unataka kuondoa attention ya Watanzania katika serikali ya JK? Atake asitake, JK ataandamwa kwa kuwa alizitafuta kura kwa bidii kwa miaka 10 (kama alivyosema mwenyewe huko Ulaya). Tunachotaka kuona watz ni matunda ya kazi, si tabasamu na ahadi. Kama na wewe ni kibaraka wake, bahati mbaya.

Wanaomsema wanamtakia mema, si mabaya. Wanataka afanye kazi, si kumrembaremba na sifa asizokuwa nazo. Kama unamtaka Mbowe subiri zamu yake. Si sasa. Nadhani Ngurumo hilo analijua vema. Kwani alipokuwa anamsema Mkapa katika RAI, Mbowe na Kikwete hawakuwapo? Mbona hakuwasema? Huyu jamaa yuko focused. najua kazi anayofanya. watu mbumbumbu wanabaki kukodoa macho na kuhoji eti mbona hamkosoi Mbowe! Mbowe? Hapa si mahali pake. Si rais wetu. Haongozi serikali na hatutozi kodi.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'