Sunday, July 20, 2008

Serikali, vibaka wa MwanaHALISI


Kwanini serikali na "vibaka" wamekuwa wanavamia ofisi za gazeti la MwanaHALISI? Kuna mradi gani unaowaunganisha serikali na vibaka katika ofisi hizi?
Katika picha ni Mhariri Mtendaji wa Hali Halisi newspaper, Saed Kubenea (kushoto) akizungumzia tukio la polisi waliovamia ofisi yake kwa upekuzi hivi karibuni. Kulia ni mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Sakina Datoo, katika mazungumzo na waandishi wa habari Dar es Salaam. Picha na Tryphone Mweji wa IPP MEDIA.

1 comment:

mwampondele said...

Kwanza pole sana Mkurugenzi wa MwanaHalisi kwa kupekuliwa na hawa Makachero(Watunza Mafisadi), kwa kweli Serikali ya awamu ya Nne imekata tamaaa ya kuongoza wananchi kuelekea kwenye mipango ya kuleta maendeleo ili kujikwamua katika dimbwi la umasikini. Hawa Makachero wa Tanzania wanampekua Mtu ambaye anaisaidia serikali katika kupambana na Ufisadi na wanatunza na kuwahenzi MAFISADI wenye dhamiri mbaya ya maendeleo ya nchi yetu.Makachero wa TZ hawajui kazi zao za kufanya kwa ajili ya faida ya Taifa kama kufichua Wafisadi(Meremeta, Tagold, TTCL, EPA,Kiwira Mine na TICTS, BOT Ajira za watoto wa vigogo, Reli ilivyobinafisishwa kwa kupewa wahindi ambao hana sifa za uwekezaji, Nk).Mungu tusaidie ili utuonyeshe njia kwani Serikali yetu imepotea haijui inakoelekea.Mwisho nazidi kukupa moyo Bw. S. Kubenea kuwa tuko pamoja kukuombea ili uzidi kuleta ukombozi wa maendeleo wa wananchi wote sio kwa Mafisadi Tu. mungu ibariki, Afrika, Tanzania na Gazeti la MWANAHALISI. AMENI.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'