Thursday, March 19, 2009

Hoja hii ni muhimu

Nakubaliana kabisa na hoja hii ya Dk. Willibrord Slaa. Wewe je?

4 comments:

Reggy's said...

Ni mawazo ya umaskini tu. Unapobishania maslahi, fikiria njia za kupandisha ya kwako au ya watu wengine unaowatete...si njia za kushusha ya wengine walioko juu. Kila mtu anataakiwa kupata amaslahi manono. Why wabunge? Ukipunguza ya wabunge yawatasaidia walimu au watumishi wengine wangapi?

Ansbert Ngurumo said...

Ndiyo Reggy, nakubaliana nawe kwamba ni mawazo ya maskini katika nchi maskini iliyojaa raslimali. Maskini husaidiana kwa kushirikiana umaskini na kubebeana mizigo. Na lazima uwe na mahali pa kuanzia. Labda huyu kaona aanzie kwa wabunge kwa sababu ndipo alipo, na aanze na walimu (labda ndicho kipaumbele chake). Baada ya hapo utagundua kwamba tutakuwa tumepata funzo kuwa serikali inaweza kubana matanuzi yasiyo ya lazima ili kuongeza vipato vya watumishi wa serikali bila kutegemea mikopo na misaada kutoka nje. Kama walio chini hawana uwezo wa kupanda kuwafuata walio juu, na kama inabidi tusafiri wote, inabidi walio juu washuke na kuwashika mkono walio chini. Labda Dk. Slaa najaribu kushuka. Tumkatishe tamaa?

Juma said...

Moto wa ukubwa wa posho za wabunge wasambaa Afrika Mashariki

Na Julieth Kulangwa

SIKU chache baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk WiIlibrod Slaa kutaka posho za wabunge nchini zipunguzwe, hoja hiyo sasa imesambaa karibu nchi zote za Afrika Mashariki.


Wakati, Dk Slaa akisema wabunge wanalipwa fedha nyingi kwa siku wanapokuwa kwenye vikao vya bunge ambazo alisema zingeweza kusaidia mambo mengine ya maendeleo, wabunge wa Kenya wameingia katika mgogoro na wananchi baada ya kukataa mishahara yao isikatwe kodi.


Suala hilo limezuia mjadala mkubwa ambao sasa unaelekea kuisambaratisha serikali ya umoja wa kitaifa iliyoundwa nchini humo.


Nchini Uganda, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NRM, Alhaji Moses Kigongo, alipendekeza mishahara ya kufikia Sh200,000 za nchi hiyo. 
Alhaji Kigongo alisema kupunguzwa mishahara ya wabunge, kutapunguza tatizo la wabunge kuwapatia rushwa wananchi wa Uganda wakati wa uchaguzi. 
Alisema inasikitisha kuona wabunge, wanawaahidi wananchi mambo mengi wakati wa kampeni za uchaguzi, lakini wakichaguliwa huyasahau majimbo yao na ahadi walizotoa.


Hata hivyo, mgogoro huu wa malipo ya wabunge haujaishia katika nchi za Afrika Mashariki bali umezikumba nchi za Ulaya.


Hivi karibuni, Spika wa Bunge la Ugiriki, Dimitris Sioufas alipitisha ombi la kutoongezwa kwa mishahara ya wabunge kwa mwaka huu na kupunguza kiwango cha sasa cha mshahara kwa asilimia tano na fedha zilizopunguzwa zinaingizwa moja kwa moja kwenye mfuko wa kusaidia jamii unaoitwa 'Social Cohesion Fund'.


Naye Rais wa Iceland, Olafur Ragnar Grimsson ameshaliomba bunge kuidhinisha pendekezo lake la kupunguzwa mishahara ya wabunge wa nchi hiyo kwa asilimia 15.


Nchi nyingine ambazo ziko katika mchakato wa kupunguza mishahara ya wabunge ni Malawi, Ukraine, Canada na Uingereza.


Tanzania inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinatokana na kuyumba kwa uchumi wa dunia, hivyo watu kadhaa na baadhi ya wabunge wanapendekeza kuwa posho za wawakilishi wa wananchi hao zipunguzwe.


Mapema wiki hii, Dk Slaa alipendekeza kuwa fedha zitakazopunguzwa kwa wabunge waongezewe walimu ambao alisema wanalipwa mishahara midogo sana.


Takwimu zinaonyesha kuwa walimu wa shule za msingi hupata mshahara wa kuanzia jumla ya Sh166,199 na baada ya makato Sh141,000 wakati walimu wa sekondari ngazi ya diploma huanzia jumla ya Sh203,000 na baada ya makato Sh178,000, wakati walimu wa shahada hupata kuanzia Sh360,000 na baada ya makato Sh270,000.

Mwananchi: 21.03.2009

Anonymous said...

Ongeza na hii hapa:

Wakati huohuo, Dk Slaa amemtaka Samuel Sitta kujivua nafasi zote za uongozi kwenye chama tawala, CCM ili aweze kutenda haki akiwa spika wa Bunge la Tanzania.


Dk Slaa alisema Spika Sitta ana nafasi nzuri ya kulisaidia taifa, lakini kutokana na kumezwa na CCM, amekuwa akitetea chama badala ya wananchi.


"Juzi nimesema posho za wabunge zipunguzwe, Sitta analalamika kuwa naingilia haki za bunge sasa leo nasema tunalipwa jumla ya Sh7 milioni kwa mwezi, acha posho za bungeni. Kweli hii ni halali kwa taifa masikini kama Tanzania," alihoji Dk Slaa.


Alisema malipo ya ya Sh135,000 kwa siku na ya Sh7 milioni kwa mwezi ni makubwa mno kwa wabunge kwa kuwa wafanyakazi wengi na Watanzania wanalipwa mishahara midogo na hivyo kuishi maisha duni.


"Mamilioni haya ya fedha kwenda mifukoni mwa watu ni aibu kwa nchi. Chadema tunasema hapana! Fedha hizi ziende katika masuala ya kusaidia jamii na kuongeza mishahara ya walimu, polisi, mahakimu na watendaji wengine," alisema Dk Slaa.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'