Tuesday, March 17, 2009

Wananchi wachukua Ikulu Madagascar

Ndo hivyo! Rais Marc Ravalomanana wa Madagascar ameondolewa madarakani. Alipewa muda aondke mwenyewe kwa hiari, akashindwa kusoma alama za nyakati. Sasa yametimia! Jeshi limeingilia kati, na aliyekuwa kiongozi wa upinzani, Andry Rajoelina (34) kaingia Ikulu. Ona hapa eti wanaondoa mapepo ya Ravalomanana Ikulu!

1 comment:

Subi said...

Haya, na tusubiri tuone, hizi serikali za kupinduana na kuwekana madarakani kwa mabavu hazijaanza leo na matokeo yake hayajawahi kuwa ya kujificha, uongozi katika nchi nyingi za Afrika badoni wa mgogoro tu. Sijui mwisho wa haya yote utakuwa lini watu wakaendelea na shughuli zao za maisha. Tusubiri tuone.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'