Friday, March 13, 2009

Wapime watawala wetu kwa swali hili dogo

UKITAKA kujua uwezo au udhaifu wa viongozi wetu waulize maswali. Wala yasiwe magumu. Maswali mepesi tu yanatosha kuonyesha uwezo na upeo wao. Bonyeza hapa utazame na kusikiliza swali dogo lilivyogaragaza wakubwa katika mjadala wa masuala ya kiuchumi.

5 comments:

Bwaya said...

Ngurumo,

Ushuhuda bayana umetupa
Saini wenyewe wameweka
Kuonyesha kweli ilo'bayana...
Kuwa tusipopiga kelele
Tusipopaza sauti
Tusipoamua kuwaghasi
Hakika yake korongoni watatutumbukiza...!


Walibeza
Walisonya...
Wakajidai kulala
Wakashindwa
Kelele zikazidi
Kelele zikapenya...

Sasa ona wanaumana,
Wenyewe kwa wenyewe wanachomana

Oneni wanavyoaibishana,
Hadharani wanatukanana,
Kila mmoja yake kauli,
Kelele zimewaumbua

Wapinzani heko na wapewe,
Waandishi tuzo na washikishwe,
Ngurumo mbele akiwatangulia


Hima na tuwasoteshe
Mparaganyo tuwasababishie
Kaya na tuikomboe

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Bwaya kumbe ushairi unauweza eeh! Tena ule wa kimapokeao - umepanga na vina kabisa. Safi.

Je, tuna mfumo mbadala? Au tunalaumu tu na mwingine akija kwenye usukani mambo ni yale yale. Sidhani kama kukosea kujibu swali ndiyo kipimo hasa cha uwezo wa kiongozi. Ni nani ajuaye kila kitu? Juzi juzi hapa kiongozi mmoja msomi na makini hapa alishangaa sana aliposikia kwamba kuna animal husbandry hapa Florida. Alihoji imekuwaje watu huko Florida wanaoa na kuolewa na wanyama? Je, tuyasahau yote mema aliyotenda kwa vile tu kaboronga (tena kwa 100%) hili swali?

Ali said...

MASANGU, hili swali aliloulizwa Kikwete likamshinda ni kipimo kizuri sana. Sisi tutajuaje kama viongozi wetu wanajua matatizo yetu? Tutajuaje kama wana uwezo wa kuyatatua? Ni rahisi kusema watajua ufumbuzi kama hawajui misingi ya matatizo yenyewe?

Sasa kwa swali hili, Kikwete alipaswa KUJUA na KUSEAMA serikali yake INAFANYA NINI katika suala la wawekezaji na sekta binafsi ili kulinda nchi dhidi ya maangamizi makubwa ya kiuchumi. Ni mawili ama anajua auu hajui. Tena zaidi ya hapo ni ama serikali inafanya kitu au haifanyi kitu.

Kkwa jinsi alivyojibu, Kikwete hajui serikali inafanya nini katika suala hili. Kama hajui yeye ni kiongozi wa serikali ipi? Tunachojua ni kwamba kuna kitu serikali inafanya. Lakini kinachosikitisha ni kwamba rais wetu hajui inafanya nini.

Kujikanyaga mbele ya umma kiasi hiki si sifa ya kiongozi yeyote. Hili ni swlai lilihitaji majibu ya 1, 2, 3, 4, 5. Majibu yake yakubabaika ni ishara ya uwezo mdogo, ujuzi mdogo, na ule usanii ambao wananchi wanazungumzia kila mara. Sidhani kama kuna haja ya kumtetea hapa mtu wa aina hii. Au shikaji wengine mnaona hii ni sifa?

Bwaya said...

Jingine linalotia hofu Masangu...


Juzi wamekuja wanafunzi wa Ujerumani
Mwenye kaya kawaitia magogoni
Pasi kusita wakamwasha Mkubwa utosini
Kijiswali mle sebuleni...


Iweje nchi nyeusi Nyuma ziwe kiasi hiki...
Wakati 'ndege zapaia' ughaibuni na udosini?

Unajua alijibuje?
Kadiria jibule
Zawadi nkugaie...

Vuu pumzi nilivuta
Hamu ilinikata
Luninga nkaizima
Kichwa nkatikisa...

Ansbert Ngurumo said...

Masangu utajuaje kuna mfumo mbadala kama kila mtu yuko cynical? Kwani hawa wa CCM waliupata wapi wa kwao (uliochoka) ambapo wananchi wengine hawawezi kuupata? Kwani CCM wanba monopoly ya akili na ubunifu? Huoni kwamba cynicism hii ndiyo inatunyima fursa ya kufanya mabadiliko? Yaani kundi hilo dogo ndilo lililosoma, linalijua, linaloipenda Tanzania kuliko mamilioni ya Watanzania waliobaki? Mbona kila mtu anajua wameshindwa? Tunataka ushahidi gani?

Sikiliza: nchi ambazo wananchi wameendekeza mawazo kama haya jeshi limeingilia kati na kufanya mapinduzi, na kwa asilimia kubwa yamekuwa maafa. Lakini angefanyaje kama wananchi wenyewe hawataki kuthubutu wanaishia kutiliana shaka, na hawataki kuondoa tatizo? Hii ndiyo changamoto inayowakabili Watanzania. Naamini kwamba Tanzanoa bila CCM inawezekana.

Haya unayouliza hapa yamekuwa yakitumiwa kukataa mabadiliko katikanchi nyingi. Kenya walisema hivi hivi kwamba nani kama KANU? Kuna watu hawakuona kama kuna kitu kitawezekana bila KANU hadi kina Raila walipojitokeza na kusema 'hapana!'

Ni kweli, si kila kiyu kimekwenda kama walivyotaka lakini yapo mabadiliko ya kimsingi yamefanyika. Na yamegomagoma kwa sababu waliochukua nchi ni wale wale tu - Kibaki na Moi ni zao la mfumo ule ule, nawamewahi kuongoza pamoja. Lakini kuna hatua wamepiga, na mfumoi mkongwe umelegezwa! Bado sisi.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'