Monday, March 09, 2009

Kabumbu: Kumbukumbu Muhimu

Wapenzi wa soka mtakaoweza kutazama mechi hizi, nawaletea kumbukumbu za mechi chache muhimu za Kombe la Dunia. Mnaweza kuanza na hii iliyochenzwa na akina PELE mwaka 1970 muone Brazil ilivyoichapa Italia; usipitwe na bao la 'Mkono wa Mungu' lililofungwa na Maradona katika fainali za mwaka 1986; itazame mechi bora kati ya Brazil na Ufaransa mwaka 1986; fuatilieni tathmini fupi ya Kombe la Dunia mwaka 1998 na kifafa cha Ronaldo de Lima.

Linki hizo hapo zinafunguka vema kwa walio Uingereza. Walio nje ya Uingereza nao wanaweza kutumia lakini inabidi wajipatie proxy server ya bure ya UK na wawe na kaufundi kiasi ka kuifiksi. Wale walio Marekani, kama wanatumia Intaneti yenye kasi kubwa wanaweza kufaidi uhondo huu kupitia ESPN360. Vinginevyo, nenda Yahoo World Cup Coverage.

2 comments:

Subi said...

Watu wa UK mnajipendelea eeh? haya bwana. Mnatunyima wengine kuona hizo kumbukumbu jamani. Nimejaribu kutizama hizo linki saiti ya BBC wakanirushia mkwara kuwa, "We are sorry but this content can only be viewed by users inside the UK."

Ansbert Ngurumo said...

Subi, pole! Ndo ubaguzi huo. Si unajua tena? Lakini nadhani kuna ufumbuzi. Ngoja nifuatilie.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'