Sunday, September 05, 2010

Slaa ataka Watanzania wapate 'Slaa' mwingine Bungeni

Mgombea urais kupitia Chadema Dk. Willibrod Slaa amewataka wananchi wa Singida Mashariki kumchagua Tundu Lissu kuwa mbunge wao, ili kuziba pengo lake (Slaa) ambaye baadhi ya wananchi wamekuwa wakimlilia kwamba angebaki Bungeni kuwatetea. Dk Slaa alisema Tundu ni kiongozi jasiri, ambaye iwapo atakuwa katika Bunge na Halmashauri atatetea maslahi ya wananchi wote, kama alivyofanya Dk. Slaa kwa miaka 15 mfululizo. Dk. Slaa alisema hayo wakati akimnadi Lissu katika mikutano ya hadhara jimboni mwake, kwenye maeneo ya Makiungu, Dung'unyi, Ntuntu na Mang'onyi mkoani Singida.

3 comments:

malkiory said...

Wale watanzania wafinyu wa mawazo waliowahi kutoa maoni yao kuwa Slaa hakustahili kugombea urais kwa kigezo kuwa bunge lingezubaa sasa wamepata jibu kuwa Slaa si mtu pekee bali akina TUNDU LISSU!

Stella said...

Wako akina Slaa wengi; hawajapewa nafasi tu. Yupo John Mnyika, hata mwenyekiti wa CHADEMA Mbowe, ni dizaini ya Slaa. Wote hawa wakishirikiana na wapambanaji wengine kama Zitto, Halima Mdee, Ahmadi wa CUF, etc bunge litawaka moto. Jambo lililopo mbele yetu ni kuwachagua ifikapo tarehe 31 Oktoba.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'