Dk Willibrod Slaa ameshapiga kura nyumbani kwake, Karatu; na sasa yuko njiani kuelekea Dar es Salaam kusubiri matokeo.
Hapa chini watazame Maalim Seif na Jakaya Kikwete wakipiga kura zao pia.
Tunahitaji kujua kwa sababu hatujui; na hatuwezi kujua kama hatujui kwamba hatujui...Hatutajua chochote iwapo hatutahoji na kudadisi. Na kadiri tunavyojua, ndivyo tunavyogundua kwamba hatujui...
Sunday, October 31, 2010
Hivi ndivyo Dk Slaa alivyofunga kampeni Mbeya
Picha ya kuchora inayomwonyesha pamoja Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Dk Willibrod Slaa, iliyochorwa na Kasambara Joseph na Salim Ahamed. Dk Slaa alikabidhiwa picha hiyo katika mkutano wake wa kufunga kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Ruanda Nzovwe jijini Mbeya, jana 31/10/2010
Pichani, Goodluck Haule, aliyekuwa mwanachama wa CCM, akimkabidhi Dk Slaa moja ya mavazi ya CCM baada ya kukihama na kujiunga na Chadema jana mjini Mbeya.
Wafuasi na wanachama wa CHADEMA wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za Dk Willibrod Slaa uliofanyika kwenye Uwanja wa Ruandanzovwe jijini Mbeya 30/10/2010
Monday, October 25, 2010
Dk Slaa awa kivutio Zanzibar
Friday, October 22, 2010
Slaa nyumbani kwa Lowassa
Hana kawaida y akupokea kadi za wana CCM wanaohamia Chadema, lakini naona hapa ameamua kuvunja mwiko. Katika picha hii, Dk Slaa amesimama na Amani Mollel ambaye ni mgombea ubunge wa Monduli kupitia Chadema, wakizichambua kadi za wana CCM 46 wa Monduli waliojiunga na Chadema kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Bomani Polisi, Monduli mjini, mkoani Arusha.
Dk Willibrod Slaa akimpongeza mmoja wa kati ya vijana 46 wa kimasai wa Jimbo la Monduli waliojiunga na chama hicho wakitikea CCM, kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Monduli, mkoani Arusha
Dk Willibrod Slaa akiwahutubia wakazi wa Monduli mjini kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo Ijumaa asubuhi kwenye Uwanja wa Bomani Polisi mjini humo mkoani Arusha
Dk Slaa 'afanya kufuru' Mwanza
Monday, October 18, 2010
Slaa katika picha Bukoba - Kahama
Dk. Willibrod Slaa akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Kahama mjini Kahama, mkoani Shinyanga jana jioni.
Dk. Willibrod Slaa akisalimiana na baadhi ya watawa waliohudhuria mkutano wa kampeni zake kwenya Uwanja wa Sabasaba mjini Nzega jana asubuhi.
Sehemu ya wakazi wa Nzega wakiagana na Dk. Willibrod Slaa mara baada ya mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Sabasaba.
Dk. Willibrod Slaa akihutubia katika mkutano wake wa kampeni kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Nzega, Tabora.
Dk. Willibrod Slaa akihutubia wananchi wa kijiji cha Mganza, Jimbo la Chato.
Akinana mama wakazi wa mji wa Bukoba nao hawakuachwa nyuma katika mkutano wa kampeni za Dk Slaa mjini Bukoba. Katika picha hii wanalea watoto wao, huku wakimsikiliza Dk. Willibrod Slaa katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa (UHURU).
Dk. Willibrod Slaa akihutubia wakazi wa mji wa Bukoba na vitongoji vyake katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Uhuru.
Monday, October 11, 2010
Slaa: Sitaki Urais wa Damu
Akiwa mwishoni mwa ziara yake mkoani Kigoma, Dk Slaa aliwataka wananchi kujihadhari na CCM na Kikwete kuhusu kauli za kuwamga damu zinazosambazwa na wanapropaganda wa CCM. Hii ndiyo kauli yake:
“Mimi sitaki kwenda Ikulu kwa kumwaga damu ya Mtanzania yeyote. Sijatamka hata siku moja kumwaga damu. Nataka uchaguzi wa amani na utulivu. Katika mikutano yangu zaidi ya 400 niliyofanya sasa, nimehimiza watu wangu kuzingatia amani…Nyie mkipigwa shavu hili geuza jingine, msiwe chanzo cha vurugu.
“Amani haihubiriwi, bali inajengwa kama vile Chadema inavyowajenga Watanzania katika sera zake. Tunaposema kutoa elimu bure, afya bure na kuboresha makazi ni kwa faida ya Watanzania wote, hatutaki kujenga matabaka….Lakini CCM imekuwa inapeleka vijana wake kwenye makambi kujiandaa kufanya fujo…Lakini wajue kuwa amani itakuwapo kama haki itatendeka.
Thursday, October 07, 2010
Dk Slaa akiwa Tunduma, Namanyere
Dk. Willibrod Slaa, akihutubia wakazi wa mji mdogo wa Namanyere katika Jimbo la Nkasi Kaskazini mkoani Rukwa, akiwa njiani kuelekea Mpanda nyumbani kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Kwa mujibu wa Evarist Shija, mmoja wa maofisa wa serikali waliohudhuria, JK alipofika hapa alipata karibu nusu ya umati huu, licha ya kuwasomba kwa mabasi na malori kutoka sehemu za mbali, tena baada ya matangazo ya nguvu.
Dk. Willibrod Slaa akihutubia maelfu ya wakazi waa mji wa Tunduma, katika mkutano wake wa kampeni, kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma
Sehemu ya maelfu ya wakazi wa mji wa Tunduma, wakipunga mikono kumpokea Dk. Willibrod Slaa, alipowasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma.
Monday, October 04, 2010
Dk Slaa akiwa Singida na Mbeya
Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Mbalizi mkoani Mbeya, wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali, wakati wa mkutano wa Dk. Willibrod Slaa.
Mgombea ubunge katika jimbo la Mbeya Mjini kupitia CHADEMA, Joseph Mbilinyi (Mr Sugu), akiwatumbuiza wananchi wa mji wa Mbalizi, wakati wa mkutano wa Dk. Willbrod Slaa.
Dk. Willibrod Slaa akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mbalizi mkoani Mbeya, kwenye Uwanja wa Stendi ya Mabasi.
Mkuu wa wilaya ya Mbarali, Kanali Mstaafu Cosmas Kayombo (aliyeketi kulia), akisikiliza mkutano wa kampeni wa Dk. Willibrod Slaa katika eneo la Chimala mkoani Mbeya.
Mgombea ubunge Jimbo la Iringa kwa tiketi ya Chadema, Mchungaji Peter Msigwa akijinadi kwa wananchi mbele ya Dk Slaa.
Subscribe to:
Posts (Atom)
- Ansbert Ngurumo
- Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'