Monday, October 04, 2010

Dk Slaa akiwa Singida na Mbeya



Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Mbalizi mkoani Mbeya, wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali, wakati wa mkutano wa Dk. Willibrod Slaa.



Mgombea ubunge katika jimbo la Mbeya Mjini kupitia CHADEMA, Joseph Mbilinyi (Mr Sugu), akiwatumbuiza wananchi wa mji wa Mbalizi, wakati wa mkutano wa Dk. Willbrod Slaa.



Dk. Willibrod Slaa akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mbalizi mkoani Mbeya, kwenye Uwanja wa Stendi ya Mabasi.



Mkuu wa wilaya ya Mbarali, Kanali Mstaafu Cosmas Kayombo (aliyeketi kulia), akisikiliza mkutano wa kampeni wa Dk. Willibrod Slaa katika eneo la Chimala mkoani Mbeya.



Mgombea ubunge Jimbo la Iringa kwa tiketi ya Chadema, Mchungaji Peter Msigwa akijinadi kwa wananchi mbele ya Dk Slaa.

3 comments:

Stella said...

Je umati wote huu unaohudhuria kampeni utampigia Dr. Slaa kura ya NDIYO ifikapo 31 Oktoba? Hilo ni jambo moja, lakini la pili, na linalofanana na hilo ni je? endapo watampigia, kura hizo zitasalimika na wizi wa CCM? CHADEMA kimejizatiti vipi kuzilinda kura hizo?

Dr. Slaa, anza kuhutubia wasikilizaji wako kwa kujitanabaisha na chama. Kwa kufanya hivyo utaiondoa dhana ya u-mimi inayoelekea kujijenga katika hotuba na kauli zako. Sema chama chako kinasema nini; isiwe wewe ndiye unayesema, hapana, unatujengea hisia kwamba CHADEMA kinaongozwa na fikra, mawazo, maamuzi, etc yako wewe kama wewe.

Mkoa wa Pwani tunakusubiri, hasa huku nyumbani kwa JK - fika hata uzungumze nasi

Anonymous said...

Naitwa Mujuni naishi Ifakara.
Nimesikia mara kwa mara chama tawala kikisema kuna mgombea alisema kumwaga damu. Kwa kuelewa kwangu nikahisi CHADEMA ndio kinalengwa! Kinacho nishangaza ni kwa nini sijasikia CHADEMA wakijibu kuhusu suala hilo. Ombi langu CHADEMA iteni press conference mtueleze kinachoendelea na tumia hata mikutano ya kampeini iliyobaki kufafanua jambo hilo. Sitegemei na siwazii CHADEMA kuwa na jaribu la kutoa kauli kama hiyo. Tunaomba ufafanuzi tadhali.

Stella said...

Ndugu Mujuni wa Ifakara, hapana, ninavyojua mimi (I stand to be corrected) aliyetoa kauli juu ya 'damu itamwagika' ni Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Bwana Mbatia, kwenye mkutano wa kampeni za ubunge kule Kawe. Jihabarishe zaidi kwa kutembelea Gazeti la Majira la tarehe 25 Septemba, kama sikosei. Huko utakutana na 'story' ya Peter Mwenda.

Kama wapo wengine ambao wameshatoa kauli kama hiyo - ulivyosema wewe kuwa unafikiri ni Dr. Slaa, hapo tena itakuwa news kwangu na huenda na kwa wengine walio gizani kama mimi. Lakini itoshe tu kusema kuwa mwenye kauli yake ni Mbatia na ndiyo sababu CHADEMA imekuwa, inaendelea na itaendelea kuhubiri AMANI.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'