Thursday, September 02, 2010

Slaa amrudi Makamba

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa, amesema kuwa vigogo wa CCM hawana ubavu wa kumnyooshea kidole kuhusu maisha yake binafsi. Akihutubia wananchi katika mji wa Babati, mkoani Manyara, Dk. Slaa alisema iwapo wataendelea kuacha masuala ya kitaifa na kujihusisha na maisha yake binafsi, naye atawavaa na kuwavua nguo mmoja baada ya mwingine, kwani anawajua. Na kwa kuanzia, alimtaka Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, awaeleze Watanzania kwa nini alifukuzwa ualimu wa shule ya msingi. Dk. Slaa alisema yeye hakufukuzwa upadri, kama Makamba anavyodai; bali aliamua kuacha kwa kufuata sheria za kanisa, na akapewa kibali kutoka Vatican kinachomruhusu kuwa mlei na kuoa. Alisema iwapo Makamba atadanganya wananchi kuhusu kilichosababisha afukuzwe ualimu, Dk. Slaa atamuumbua. Habari za uhakika zinasema Makamba alifukuzwa ualimu (mkuu) wa shule kwa kosa la kumbaka na kumpa mimba mtoto wa shule.

Naye Mkuu wa msafara wa Dk. Slaa, Suzan Kiwanga, alimtolea uvivu mke wa rais, Salma Kikwete, akisema anatumia pesa za umma kuzunguka nchi nzima anafanya kampeni huku akijua kuwa hatambuliki katika ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kauli ya Kiwanga iliongezewa uzito na Dk. Slaa aliyesema: "Nchi hii ina rais mmoja, ni Kikwete. Mke wa rais si rais. Anatembea kwa msafara wa magari 21 huku akilindwa na kupewa heshima zote na viongozi wa serikali; kama nani? Na raisi mwenyewe atatumia magari mangapi? Lakini hii yote ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi, na huu ni ufisadi," alisema huku akishangiliwa na umati uliokusanyika katika uwanja wa Kwaraha mjini babati.

Ilisemekana kwamba, asubuhi ya leo, kabla ya mkutano wa Dk. Slaa, Salma alitaka kuuteka uwanja huo na kuutumia kwa mikutano yake ya hadhara, lakini wananchi wa Babati wafuasi wa Chadema walimtolea macho na kumfukuza uwanjani hapo. Hali hii ndiyo ilisababisha kauli ya Kiwanga, ambaye alisema: "Laiti ningemkuta hapa, sementi hii (sakafu) ingegeuka vumbi." Akasisitiza kwamba kama Salma angekuwa anataka kufanya siasa, angechukua fomu agombee urais kama mumewe ili apate fursa ya kuzurura na kufanya mikutano. Lakini si vema kutumia pesa za Ikulu au za asasi yake ya WAMA kufanya siasa.

3 comments:

Stella said...

Hapa ndipo patamu!

Watu walishaonya kuhusu tabia ya Makamba kusema hovyo na hasa kuwahusu wapinzani. Akitaka kuitetea CCM anaboronga; akitaka kuukandia upinzani anaboronga zaidi; sasa watu 'watasinya' kweli!

Ushauri wa bure kwa Makamba ni kukaa kimya ili watu wanaofahamu kwa uhakika kabisa mambo yake wamsitiri na aibu itakayomkuta pale watakapoamua kuyatoa hadharani.

Hivi huyu Katibu Mkuu wa CCM alichaguliwa kutokana na sifa zipi hasa? Hivi kweli CCM hawakujua kuwa Makamba ni mmoja wa wabakaji wa watoto wa shule?

Walimchagua kutokana na sifa ya maneno mengi yasiyo na mantiki? Maneno ya kuumbuana? Au ya kupashana? Labda ni swali gumu - lakini Kikwete na CCM yake anajua majibu yake. Duh! Mzee huyu!

Amri Musa said...

CCM wamekosa nguvu ya kisera, wameamua kuingia katika suruari za wananume wenzao. Wanatafuta nini? Wakumbuke kuwa upande mwingine nao ukiamua kwenda kwa staili hiyo, watakaoumia ni CCM, hasa Rais Kikwete kwa sababu amefungua mno zipi ya suruali, na amesababisha madhara mengi. Acha waendelee uone kitakachozaliwa humu!

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'