Thursday, October 11, 2012

Naibu Waziri Wa Sheria Na Katiba Akiwa Ghana

Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angela Kairuki akiteta na Naibu Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Dk. Arthur Mutambara katika kongamano la mwaka la wajasiriamali na viongozi wanaochipukia Barani Afrika, linalofanyika kwa siku tatu Accra, Ghana, kuanzia jana. (Picha na Ansbert Ngurumo)

Ngurumo Ahudhuria Mafunzo Accra Ghana


Mkurugenzi Mtendaji wa Vox Media, ambaye pia ni Naibu Mhariri Mtendaji wa Free Media, Ansbert Ngurumo, akiwa miongoni mwa washiriki wa kongamano la mwaka la wajasiriamali na viongozi wanaochipukia Barani Afrika, linalofanyika Jijini Accra, Ghana, kwa siku tatu kuanzia Jana.

Friday, September 28, 2012

Magamba Yapukutika Nyakatanga

Baadhi ya makumi ya wana CCM wameamua kuvua magamba na kujiunga na M4C mbele ya Ansbert Ngurumo aliye Muleba pamoja na John Heche kwenye M4C

Heche Aendeleza M4C Kamachumu

Leo John Heche Mwenyekiti wa CHADEMA viana taifa,akiwa Kamachumu,Muleba, kagera

Sunday, September 23, 2012

John Heche Apenya Vijiji Muleba




 Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Heche, akihutubia Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nsisha, Kagoma, Wilayani Muleba, Mkoa wa Kagera.
 Wananchi
 Katibu wa CHADEMA Muleba kaskazini


John Heche na viongozi wa jimbo la Muleba kaskazini

Monday, September 17, 2012

Hotuba ya Mbowe Washington DC

Mheshimiwa Freeman Mbowe akihutubia Watanzania waishio Marekani kuhusu azima ya mabadiliko Tanzania. Anasema mabadiliko yanayotokea sasa ni mpango wa Mungu! Msikilize sasa.

Wednesday, September 05, 2012

Tuesday, September 04, 2012

Tanzia mwanana ya Daudi Mwangosi

Katika yote yaliyoandikwa kuhusu mateso na kifo cha Daudi Mwangosi (pichani) aliyeuawa na polisi kijijini Nyololo, Iringa, andiko hili linastahili enzi ya pekee, na linastahili kuwa tanzia mwanana ya Hayati Mwangosi. Requiem In Pacem!

Thursday, July 19, 2012

Nukuu ya Leo kutoka UN

“Neither peace, development nor human rights can flourish in an atmosphere of corruption.”(Amani, maendeleo au haki za binadamu haviwezi kushamiri mahali penye ufisadi) - Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

M4C yavuna mamia Chato kwa Magufuli

Mmoja wa mavuno mapya ya M4C ni Dk. Benedict Lukanima, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe. Ndiye aliyenipokea na kunionyesha mazingira katika Chuo Kikuu cha Hull, Uingereza; wakati huo akiwa katika mwaka wa pili wa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Uchumi.

Wednesday, July 18, 2012

Nukuu ya Sugu Bungeni

"Natuma salamu kwa Kova kwamba ile filamu yake ya Dk Ulimboka, Mchungaji, na Mkenya, wananchi hawajaielewa; hivyo ni vema arudi Studio ili afanye remix!" Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema)


Sunday, July 08, 2012

Nukuu ya Leo

"Katika mapambano ya ukombozi ni lazima wengine wawe mbegu, sisi tupo tayari kufanywa mbegu.” Dk. Willibrod Slaa Julai 8, 2012: Dar es Salaam

Saturday, July 07, 2012

Libya wachagua rais mpya

Wananchi wa  Libya leo wamejitokeza kwa wingi kupiga kura kuchagua rais, katika uchaguzi huru baada ya miaka 60 ya udikteta. Habari zaidi soma hapa.

Serena ang'ara tena

Mchezaji maarufu za tenisi Serena Williams ameibuka kidedea kwa kutwaa taji mara ya tano
.

Narejea

Nimekuwa mbali na blogu hii kwa muda sasa. Nimerejea. Tarajia mwendelezo wa harakati.

Monday, April 02, 2012

Chadema kidedea Arumeru Mashariki



CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeshinda katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki. Kwa hiyo, Mbunge wa Arumeru Mashariki ni Joshua Nassari (pichani kulia). Kura halali 60,038: Zilizokataliwa 661. Wagombea: Mazengo Adam (AFP) 139; Charles Msuya (UDP) 18; TLP 18; Kirita Shauri Moyo 22; Hamisi Kiemi 35; Mohammed DP 77; Sumari, Sioi 26757; Nassari, Joshua 32,972. Vile vile, kimeshinda udiwani katika kata nyeti zote nchini. Nguvu ya Umma imefanya kazi. Mchakamchaka kuelekea 2015!

Thursday, March 29, 2012

Mexico wasaka Amani kwa Haki na Utu


Wameksiko jana waliadhimisha mwaka wa kwanza wa Harakati za kulinda Amani kwa Haki na Utu, mjini Cuernavaca. Maandamano, machozi, ngoma na ibada ni baadhi ya mapambo ya maadhimisho hayo. Dada huyu naye alikuwa kikolezo cha maadhimisho. Waweza kujisomea zaidi habari hizo kwa Kiingereza katika tovuti ya narconews. Mama huyu aliimba kwa hisia. Na kasisi huyu alisali kwa hisia pia, ingawa kusema kweli sikuwa naelewa alichosema. Lugha gongana!

Fidel Castro amuuliza Papa swali jepesi


Wote ni wazee. Wanazidiana mwaka mmoja tu. (85-84). Mmoja ni Mkomunisti. Mwingine ni Mkristo Mkatoliki. Mmoja amewahi kuwa rais wa Cuba. Mwingine sasa ni rais wa Vatican City. Baada ya Castro kufuatilia ziara ya Papa Benedict XVI kwenye runinga tangu alipotua nchini humo siku tatu zilizopita, alipopata fursa ya kukutana naye ana kwa ana, akamuuliza: "Hivi kazi ya Papa ni nini?" SOMA HAPA uone majibu ya Papa.

Monday, March 12, 2012

Oa mwanamke mzee, kufa mapema!

SI mimi ninayesema hivyo. Ni utafiti mpya. Soma hapa.
My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'