Saturday, June 07, 2008

Hii ndiyo pensheni ya Mkapa?

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amenukuliwa akisema kuwa yeye anaishi kwa pensheni kama alivyo Mzee Ali Hassan Mwinyi; kwamba hana utajiri wowote, na kwamba wanaomhusisha na biashara akiwa Ikulu na ufisadi mwingine unaozungumzwa wanamwonea kwa sababu eti alikataa kuwapendelea alipokuwa rais. Lakini Mzee Mkapa hajakanusha ujasiriamali wake wa Ikulu unaowakera wananchi. Baadhi ya yanayosemwa juu ya Mkapa, ambayo hajayakanusha kabisa, ni haya hapa. Je, hii ndiyo pensheni anayozungumzia?

3 comments:

Anonymous said...

Mkapa awadanganya watoto wadogo, amaechafua rekodi yake, hatuna imani naye tena.

Anonymous said...

Rais Mkapa amejiharibia heshima yake..Ni fisadi tu hata kama polisi watatukamata.

Anonymous said...

Waswahili husema. mwoga ukimkimbiza takimbia, lakini akichoka na kusimama, basi ujue kuna mawili: KUFA AU KUPONA.
Watanzania tumefukuzwa kiasi cha kutosha na hawa viongozi fisadi wa CCM, sasa tumechoka na tunataka haki zetu zirudi ili na sisi watoto wetu wapate angalau madawati ya kukalia shuleni, licha ya ukosefu wa dawa katika zahanati za Zinga na Nyakaliro. kikwete sasa angalia nchi isije ikawa kama Zimbabwe au Burundi. Usiwaogope hao marafiki zako, tafadhali wafikishe KISUTU KAMA ALIVYOFIKISHWA BALOZI WETU WA ITALIA.Katiba ya nchi uisome na uwe rais siyo rafiki. tumia madaraka tuliyokupa na utusaidie tuondokewe na hawa mafisadi na warudishe mali zetu.AFADHALI WAKATI WA NYERERE AU WAKATI WA UKOLONI MWEUPE KULIKO HUU UKOLONI MWUSI.

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'