Wednesday, August 25, 2010

Msafara wa Kikwete waua mtoto

HABARI zilizoifikia blogu hii jana jioni zinasema gari moja aina ya Land Cruiser VX, T 181 BJP, lililokuwa katika msafara wa Rais Jakaya Kikwete, jana liligonga na kuua mtoto pala pale, eneo la Izigo, Muleba, mkoani Kagera. Hata hivyo, wahusika katika msafara huo wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM walisema gari lililoua halikuwa katika msafara. Baadaye ilidhihirika kuwa gari hilo lilikuwa limeutangulia msafara wa JK; na lilibeba vifaa vya kampeni vya CCM. Dereva wa gari hilo alishikiliwa na kuhojiwa na polisi mkoani Kagera, lakini jitihada za kupata mamlaka husika kufafanua ajali hiyo hazikufanikiwa. Tutaendelea kuifuatilia. Mwaka 2000 msafara wa aliyekuwa mgombea wa CCM, Rais Benjamin Mkapa, ulia mtu mkoani Mwanza. Waandishi walioambatana naye waliamriwa wasiandike habari hiyo kabisa. Walibaki kusimulia kwa midomo baada ya kampeni!

1 comment:

Stella said...

Naibu Mhariri Mtendaji, Tanzania Daima, gazeti la Habarileo la leo tarehe 25 Agosti limewasha moto wa malumbano kuhusu habari ya Christopher Nyenyembe 'TUCTA: JK amechelewa'
iliyoandikwa kwenye Tanzania Daima tarehe 24 Agosti. Mgaya amekanusha kuzungumza yaliyoandikwa 'Mgaya akana kumuamrisha Kikwete
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 25th August 2010......'


Ni nani mkweli hapa!

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'