Thursday, August 12, 2010

Nyerere na Kikwete: Wanalinganishika?
7 comments:

Anonymous said...

Well done Ansbert. Niliona hizi picha jana nikazipenda kwa jinsi zinavyofungua ufahamu hasa linganifu. Ukilinganisha watu hawa wawili mjenga na mbomoa nchi unapata jibu la kura yako iende wapi kwenye uchaguzi. Tangu lini mtu akalima au kupanda akiwa kwenye mswala mke au busati kama ilivyo hapo juu? Ajabu anayefanya hivyo ni mtoto wa maskini wa kunuka toka pale Chalinze!
Kweli mwalimu Nyerere alikuwa mbele ya umri wake na ameacha mifano ambayo hakuna hata anayeweza kufikia moja ya milioni yake kwa hawa walioko madarakani wakiyafuja na kuchuma wasipopanda.
Naogopa kuandika makala nzima. Nashawishika kusema kuwa picha hizi zinatosha kuwazindua wale wanaong'ang'ania ukale na ufisadi bila kujua kuwa waliwao ni wao.
Mpayukaj Msemahovyo

Subi said...

Niliwahi kuwavuti.comlinganisha picha za wawili hawa siku moja pale nikaambiwa, 'dada, umepitwa na wakati wewe', nikasema, AMA!

Anonymous said...

Nimependa hii observation. Hawa watawala wa leo si dotcom (usanii mtupu na hawahitaji kufikiri sana kwa sababu fikira zote zinapikwa Washington DC - kinachosubiriwa ni ku-C&P copy and paste). Ninashangaa hakuvalia suti ya ulaya (suti na tai).

Yasinta Ngonyani said...

Kila kitu kinafuata nyanyo. Kwa namna yake wanalinganishika.

Anonymous said...

This is good for those with brain

John Mwaipopo said...

subi sikuwezi katika lugha.

Subi said...

John wewe, LOL ha ha ha, nakisia kilichosababisha useme hivyo, wacha nijitetee, ilikuwa bahati mbaya hapo ilipounganika 'kuwavuti.comlinganisha' baada ya kubofya kifute ndipo nikagundua nilikosea, ilitakiwa iwe 'kuwalinganisha pale wavuti.com'

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'