Saturday, August 21, 2010

Kikwete aanguka tena jukwaani


Tumpe pole Rais Jakaya Kikwete. Ameanguka jukwaani, Jangwani Dar es Salaam, siku ya ufunguzi wa kampeni yake. Niliwahi kuwauliza madaktari wa rais, walipotoa taarifa ya ugonjwa wa rais, wakasema hataanguka tena. Nikasema, iwapo ataanguka tena, watatuambia nini? Nadhani hapa kuna tatizo kubwa. Tumwombee, na tumshauri Rais Kikwete.

22 comments:

Anonymous said...

naafikiana na wewe kwamba kuna maengi ya kuhoji juu ya hali hii.

Anonymous said...

Hili swala ni nyeti! Siasa mchezo mgumu sana. Hawa watu kuna siku watakuja kuuana na mauchawi yao. Kitu chenyewe hata Doctor hakioni...hichi kitu 100% ni cha ki-wichi. Doctor hana makosa hapa ..ni kweli hakisomi kwenye vipimo vya kitabibu. Nashauri aende Bagamoyo, Sumbawanga, Kigoma na Tanga. Baada ya hapo haji kuanguka chali ten. JK

Anonymous said...

Afya ya jamaa huyu ni mgogoro ingawa yeye na madaktari wake hawataki kukubali. Tusiandikie mate hata hivy. Mwenye kuficha maradhi kilio humfichua. Usiri na usanii zimekuwa silaha kuu za Kikwete kuficha uovu na ubovu wake. Hebu angalia alivyoendelea kutotaja mali zake wakati anakabidhiwa mali za umma. Je huyu si fisadi? Inshallah Mungu atatuhukumia kama alivyofanya kwa Dito muuaji.
Mpayukaji

Anonymous said...

Maoni yangu:
1. Rais Kikwete ajitoe katika mbio hizi mapema kwani kijua ndio hichi uzipozianika utazila mbichi.
2. Wasaidizi wa rais mambo ya afya, hususani dr wake bw. mwafisi kama bado yupo ni wakati wakaachana na kazi hiyo ya kumtibu rais. walishawaahidi watanzania kuwa amiri jeshi hataanguka tena na watakuwa waangalifu... sasa inakuwaje?
3. ile mara ya kwanza 2005 ilikuwa ni uchovu wa kufunga kampeni, hii nadhani waiite uchovu wa kuanza kampeni...

na mwisho nimalize kwa nukuu yako mwenyewe:
"...Rais wetu si dhaifu kama wananchi wake ambao wengi wanalalala au kushinda njaa; wanapata mlo mara moja moja (na wenyewe haujakamilika virutubisho); wanafanya kazi nzito na ngumu zinazokula nguvu ya mwili na akili; wana pato duni sana (chini ya shilingi 1000 kwa siku); wanakabiliwa na magonjwa hatari na hawana huduma ya matibabu inayoeleweka na inayoaminika; wanaishi katika mazingira hatari; wanakabiliwa na magonjwa sugu kwa miaka mingi; wanatembea kwa miguu au baiskeli, bajaji au wanasafiri kwa malori na mabasi mabovu; hata kwa wanaosafiri kwa ndege, wanatumia madaraja ya chini yanayochosha; wanalala kwa saa 2 au tatu kila siku; wanasumbuliwa na umaskini wa kutisha kiasi kwamba kila wanapolala hawana tumaini kama wataiona kesho.

Watanzania hawa hawazimii, hawaishiwi nguvu wala hawaanguki, aanguke rais mwenye afya isiyotetereka (kama tulivyoelezwa) na mwenye matunzo ya viwango vya juu?..."

Waache utani, tuambie Rais anaumwa nini??????

Yasinta Ngonyani said...

Mungu mbariki Kikwete na pia ibariki Afrikla/Tanzania

Anonymous said...

Kuna tatizo, kama si problem!

mtakuja said...

Kikwete usihofu.Utapona tu na mchakato kama ulivyo utafanikiwa.UPONE MAPEMA

Anonymous said...

Kwanza ninampa pole sana Mh JK na tunamwombea Mungu amrejeshee afya njema.
Mimi ninafikiri hatuhitaji madaktari wake watwambie anaumwa nini. Ukweli ni kwam Mh JK ni mgonjwa kama ilivyo kwa binadamu wengine. Lakini tofauti na watz walalahoi, yeye ana 'haki' (kikatiba/kiutawala/kidola) ya kupata the best of medical service po pote pale inapopatikana. Ilibidi awe ameipata kabla ya kunza kampeni kwa vile aliishaanguka mara kadhaa uko nyuma. Bahati mbaya, wasahuri wake na yeye mwenyewe wamejenga tabia ya kutaka rangi nyekundu kuiita nyeusi. Utamaduni huu ndio umeongoza taifa na ndio unaongoza hata masuala yanayohusu afya zao! Wabadilike. Mawili: wapumzishe kampeni na aende Marekani au China akaangaliwe afya yake kwa wiki mbili au tatu. Wakiridhika arejee aendelee na kutafuta urais. Pili, akiisha ukwaa tena huo urais achukue likizo ya afya ya miezi sita akiangaliwa afya yake kwa undani zaidi, ambapo makamu wake Balali atakuwa ameshikilia madaraka wakati huo wa likizo. Hilo litatuhakikishia kuwa Rais atatimiza majukumu yake kama inavyostahiki na sisi wapiga kura hatutakuwa tumeingizwa mkenge!

Anonymous said...

Mh JK hajadondoka ila amepepesuka tu

Anonymous said...

jamani rais amefunga na kazi ya kampeni ni ngumu na huku mtu bado umefunga. jamani mnyonge mnyongeni nahaki yake mpeni mwoneeni huruma mwana wa mwenzio

Anonymous said...

jamani Siasa kila sehem??? Hata kuanguka kwake mnaanza kuchambua kisiasa?? hii ni out of topic,,

kama wote tunaamini katika mungu au chochote basi ni wajibu wetu kumuombea apone haraka.. duh wabongo tunaenda too far sometimes

Anonymous said...

Haya mambo ya secrecy kati ya Dr. na Patient haya yanazua utata.Waache uzembe la sivyo watamuua huyu Bw.mkubwa. Kama hawajiamini na utaalamu wao waombe msaada wa kiutaalam zaidi. Watanzania ONYO Msichague kwa "Kura za huruma" MWIKO tutambue kabisa kuwa mgonjwa anahitajika kukaa karibu na Madaktari ili atibiwe. Hapa tutaona kwa nje tu!! SWALI? Je, katika utendaji wake wa kila siku. Ni nini kipo nyuma ya pazia???

Anonymous said...

VIDEO CLIP YA KUANGUKA KWA KIKWETE

Hii hapa, icheki haraka kabla haijawa deleted

http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=0S2AE3xXR-Q

Anonymous said...

Ameanguka akiwa katika mkutano wa siasa. Yeye ni mwanasiasa,, na kiongozi wa kisiasa. Zaidi ya hayo, taarifa ya madaktari imetolewa kisiasa. Kwa nini tusijadili tukio hili kisiasa? Kuna kosa kumjadili mwanasiasa kisiasa? Maana hata maisha yake binafsi yana uhusiano wa moja kwa moja na siasa na nchi na uhai wa taifa.

Stella said...

Hebu Watanzania tujifunze kusema ukweli pale panapostahili kusemwa. JK anaumwa, na anaumwa kama mimi na wewe tunavyoweza kuumwa. Lakini daktari wake anataka tuamini kuwa mteja wake haumwi na kwa kutaka kuthibitisha hilo aliahidi yeye na wasaidizi wa Rais kuwa JK hataanguka tena. Tarehe 21 Agosti, ameanguka tena, Je bado tuamini hataanguka tena kwa mara ya tano?

Kujadili hapa kama Rais anaumwa au la, haitoshi. Daktari wa Rais ama hajui kazi yake, ama anatudanganya kwa kusema JK haumwi. Kwa nini aendelee kumfedhehesha Rais?

Ila hata JK mwenyewe alipofikia hatua ya kutamka neno 'aisee' wakati akiendelea na hotuba, alikuwa amekwishahisi tatizo; ndipo hapo alipopaswa kutoa ishara kwa walinzi kuomba msaada badala ya kung'ang'ania kutoa hotuba hadi fedheha imkute mbele ya umati wa watu.

Anonymous said...

Tahariri - CCM imeonyesha kampeni ya mfano, vyama vingine viige

Huenda mhariri wa Tanzania Daima (kwa siku mbili mfululizo) sasa anaanza kuyasemea mazuri ya CCM badala ya gazeti lake kuwa na makala kadhaa zinazokinzana na CCM huku zikishabikia na kusifia upinzani na hasa CHADEMA

Stella said...

Anonymous hapo juu, nina hakika wewe si mfuatiliaji mzuri wa tahariri au hata mada nyingine nyingi katika gazeti la Tanzania Daima. Wahariri na waandishi wa gazeti hili wana'balance' sana taarifa zao. Hawaangalii chama,mtu au tukio fulani tu; bali wanaangalia taarifa muhimu za kuwaarifu wananchi. Kwa maneno mengine,wanahabarisha watu kwa kila kile kilicho muhimu wajue.

Ramie said...

Jamani, kwani kuanguka kuna matatizo gani?..yeye si ni binaadamu kama wengine?..kwani tuliambiwa ukiwa rais unakuwa ni roboti au machine?..hata hiyo machine pia mara nyengine inaleta matatizo..Mbona rais wa marekani George Bush Snr naye pia alianguka?..nashuko ndio kwenye madaktari wazuri zaidi?...muacheni Kikwete atuendeshee nchi vizuri..kama kazi hiyo ni rahisi kama haya maneno mnayo bwabaja hapa..haya basi ingiini nanyinyi mukione kindubwe ndubwe!!!

Stella said...

Ni kweli Rais ni binadamu kama ulivyo wewe na mimi, na kuanguka si ajabu hata kidogo. Sawa, watu mashuhuri kama huyo Rais wa Marekani na hata Rais wa Ufaransa waliwahi kuanguka. Lakini walianguka mara ngapi? Kikwete ameshaanguka mara nne, na kwa mara tatu alianguka ndani ya kipindi kifupi sana - ndani ya miaka isiyozidi mitano.Mbaya zaidi, mara mbili zote ameanguka katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja. Kama utakumbuka vizuri mara ya mwisho alianguka kule Mwanza Oktoba 2009. Sasa hata Oktoba 2010 haijafika, Kikwete tayari ameanguka tena. Ukumbuke mara zote anaanguka mbele ya hadhira. Je Wananchi hawana haki ya kuhoji kuanguka kwa Rais wao? Tena ndani ya kipindi kifupi?. Hapana, acha wananchi wawe na wasiwasi na afya ya kikwete.

Je kuanguka kwa Kikwete kuna uhusiano na ubovu wa daktari wake?

Kazi ya U-rais ni rahisi kwa Kikwete na kwa mtu mwingine ye yote mwenye uwezo na afya njema.

Anonymous said...

We unayejiita Sleta ni nyumba ndogo ya Kikweeteeeeeeeeeeeeeeeeeeee!

Stella said...

Anonymous, blogu ni sehemu ya kutoa maoni yanayojenga. Habari za nyumba ndogo na mambo mengine yanayofanana na hayo, waachie wenye ubavu wa kuyazungumzia huko wanakoyazungumzia. Hapa si mahali pake.

Katika viwanja hivi, mwandishi wa maoni anatarajiwa kujibu hoja si kuanzisha malumbano ya maneno ya mtaani. Blogger hakuanzisha uwanja wa kashfa wala kejeli. Ustaarabu ni kitu cha bure.

Anonymous said...

ninyi binadamu mnaokejeli afya ya rais kikwete nawashangaa sana,hivi hamfahamu kama mheshimiwa rais ni binadamu kama walivyo binadamu wengine?na yeye ana mwili na roho kama kawaida sasa cha ajabu n nini yeye kupata dhoruba ya kiafya?Hebu acheni kumkufuru muumba jaman na kwa kuwa huyo ndio kiongozi wetu sisi sote tumuombee afya njema na baraka katika uongozi wake.Allah atakuepusha na wenye roho za husuda kaka yangu Kikwete.Sema amiin..!

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'