Tuesday, August 17, 2010

Serikali yatisha Maswali Magumu

JANA niliitwa Ofisi ya Idara ya Habari (MAELEZO) na kuhojiwa, nikiwa na Mhariri Mtendaji, Absalom Kibanda, juu ya ukali wa makala za Maswali Magumu ya Agosti 8, 2010 na ya Agosti 15, 2010, ambayo kwa taarifa nilizonazo yaliikera Ikulu, nayo ikaisakama MAELEZO. Kikao hicho kilishirikisha Mkurugenzi wa Maelezo, Clementi Mshana; Mkurugenzi Msaidizi, Raphael Hokororo na ofisa wa maelezo aitwaye Jovina, aliyekuwa anaandika muhtasari wa mazungumzo yetu. Tulizungumza mengi, lakini katika yote, nakumbuka nukuu ya mmoja wa vigogo hao wa MAELEZO akisema: "Mashujaa wote hawako hai...".

12 comments:

Ayoub C Kafyulilo said...

Pole mkuu!! Hata Nyerere angeogopa vitisho ni dhahiri tusingepata uhuru. Kuna kila sababu ya wachache wenye nia ya kweli ya kuikomboa nchi kujitolea kwa maslahi ya taifa. Hata kama si wao watakaofaidi matunda ya jasho na damu yao, watoto wao na vizazi vijavyo vitafaidi matunda ya makovu yenu.

Anonymous said...

UMESHAONYWA!!!!!!!!

Anonymous said...

I am sure no legal proceeding will take place against Mr Hokororo for his inhumane and immoral conduct set forth to A. Ngurumo, the message were real nasty and evil to be said by such a government official. Tunaomba sheria ichukue mkondo wake, ashitakiwe kwa tishio na uhatarishaji wa maisha ya Mwandishi wa Habari. I don’t wish any misfortune to happen to Mr Ngurumo, but what about if something wrong will happen to Ngurumo? Are we going to hesitate to associate Hokororo’s evil words? The obvious answer is no, due to a logical and causal connection.
My take: Lets the journalist society and citizens rise and defend our journalists from the malice of corrupt government officials and their cronies.
The Government should adhere to UNESCO General Conference resolution on promotion of press freedom in the world, recognizing that a free, pluralistic and independent press is an essential component of any democratic society.

Kimbache UK.

Stella said...

Ninaomba kuyasoma pia Maswali Magumu ya tarehe 08 Agosti hapa kwenye Blogu. Yaweke hapa niwe ninajikumbusha kile kilichoikera Ikulu.

Niliyasoma kwenye gazeti la Tanzania Daima. Kwa bahati mbaya gazeti la tarehe hiyo halikuwekwa kwenye mtandao.

Asante kwa kukubali.

Anonymous said...

Hongera sana kwa Kutoa maswali Magumu yanayowasumbua wale wasiopenda kutafuta ufumbuzi wa maswali. Badala yake wanatumia nguvu na vitisho. Mti wenye matunda ndio unaotupiwa mawe, kwa maana hiyo wewe ni chachu ya fikra thabiti ambazo haziwezi kuzuiwa bila hoja za kufikirika pia. Unalo jeshi kubwa nyuma yako hauko peke yako.
Kazi njema endelea kuielimisha jamii.

Reggy's said...

Sidhami maneno makali kama haya yangeweza kutolewa a vigogo hao kwa bahati mbaya. Huenda ni mawazo yao au ya aliyewatuma. Usitishike Ngurumu, endelea kuunguruma maana walilosema haliwezi kutokea kwa kuwa umma umeshawaelewa.

Stella said...

Ikulu isitishe waandishi wa habari na hasa kwa wakati 'muhimu' kama huu kwa taifa letu.

Kwako Raphael Hokororo, hata mashujaa wakifa, hawafi na ushujaa wao; bali huuacha nyuma wananchi wakautumuia kujikomboa kimawazo, kisiasa, kiuchumi, na kijamii.

emu-three said...

Mimi najiuliza kwanini mtu uogope ukweli, nafikiri mtu akikuambia ukweli hata kama unauma, umshukuru kwasababu kakuokoa!
Ina maana kweli hatufnyi makosa?
Ngoja niyasome hayo maswali kwanza, ilii nitoe hoja ya msingi

Makene said...

Siku niliyosoma maneno hayo sikutaka kuamini nilichokuwa nakisoma; machache

AMA-alitumwa (hapa anaweza kutumwa na vyote; mabwana zake au moyo wake)
-Hajui anachokisema
-Hajui Ngurumo anafanya kitu gani, hamjui Ngurumo pia
AU -Hajui namna ya kuifanya kazi yake

LAKINI kinachoshangaza kabisa ni kuwa huyo Hokororo (he is one of the so called senior journalists in the country, as far as my knowledge) hawezi kamwe kuthibitisha KUWA VIBARAKA WA WATAWALA WALIWAHI KUISHI DAIMA DAWAMU, KWA SABABU TU YA KUJIKOMBA KWA WAKUBWA NA KUWAAMBIA KUWA WANAMEREMETA HATA KAMA WAKO UCHI

Anonymous said...

huu ndiyo ukweli wenyewe"...........hata mashujaa wakifa, hawafi na ushujaa wao; bali huuacha nyuma wananchi wakautumuia kujikomboa kimawazo, kisiasa, kiuchumi, na kijamii........."
Jingo.

Stella said...

Asante ndugu Jingo kutumia tena mawazo na maneno ya Stella aliyoyaandika hapo juu ili kuzidi kuweka msisitizo wa ukweli kuhusu 'mashujaa'. Ansbert asitishwe na kauli ya Hokororo. Raphael analipa fadhila za kuweko Maelezo; haitusaidii. Raphael mashujaa wawakomboe Watanzania na nchi yao; samahani!

Stella said...

Hapo!

'Maswali Magumu' yasitishike na vitisho vya Ikulu. Yakitishika tu yatawapa mwanya wa kusema 'TUMEYANYAMAZISHA'. Badala yake yawepo ili wasomaji wa gazeti waliokuwa wanayafuatilia kwa karibu, waendelee kuyafaidi. Wengine sisi tunalipenda gazeti kutokana na sababu mbali mbali, na mojawapo ni makala.

'Maswali Magumu' rudi tukusome. Au????

My photo
Nimechongwa na mambo haya: Falsafa, Fasihi, Muziki, Habari na Harakati. Sifuati mkumbo. Napenda kuhoji na kudadisi - hulka ya kifalsafa ya kuusaka ukweli - 'UKWELI ULIO UCHI.'